TANGAZO


Saturday, June 9, 2018

Tetesi za soka Ulaya Jumamaosi 09.06.2018

Mohammed Salah akiangushwa na Sagio Ramos

Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah amesema kuwa anatumai atakuwa katika hali nzuri kuichezea Misri katika mechi yake ya kwanza ya kombe la dunia dhidi ya Uruguay mnamo tarehe 15 mwezi Juni. (Marca)
Nabil Fekiri
Image captionNabil Fekiri
Hatma ya klabu ya Liverpool kumsajili mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa Nabil Fekir haijulikani baada ya klabu hiyo ya Anfield kusita kukamilisha makubaliano hayo baada ya mchezaji huyo kufanyiwa ukaguzi wa matibabu. (Telegraph)
Klabu ya Athletic Bilbao imejiandaa kumfanya kiungo wa kati wa Manchester United na Uhispania Ander Herrera, 28, kuwa mchezaji anayelipwa zaidi huku wakijaribu kumsaini.. (AS, via Manchester Evening News)
Ander Herera
Image captionAnder Herera
Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich amekataa ombi la Jim Ratcliffe - mtu tajiri zaidi nchini Uingereza kuinunua klabu hiyo ya Uingereza. (Mail)
Kiungo wa kati wa Tottenham na Uingereza Dele Alli, 22, na mchezaji mwenza wa Denmark Christian Eriksen, 26, wanatarajiwa kufuata nyayo za nahodha wa klabu hiyo mwenye umri wa miaka 24 Harry Kane kutia saini kandarasi mpya katika klabu hiyo.(Mirror)
Wachezaji wa klabu ya Tottenham
Image captionWachezaji wa klabu ya Tottenham
Mshambuliaji wa Everton Wayne Rooney, 32, anakaribia kuandikisha kandarasi na klabu ya ligi ya Marekani baada ya kuelekea mjini Belfast ili kuweza kutuma ombi la Visa (Mirror)
Liverpool itamsaini mchezaji wa Stoke mwenye umri wa miaka 26 Xherdan Shaqiri iwapo watakubaliana kuhusu dau la uhamisho huo, kulingana na mkufunzi wa Stoke Gary Rowett. (Star)
Xherdan Shaqiri
Image captionLiverpool itamsaini mchezaji wa Stoke mwenye umri wa miaka 26 Xherdan Shaqiri iwapo watakubaliana kuhusu dau la uhamisho huo
Crystal Palace inapanga uhamisho wa kiungo wa kati wa Scotland Stuart Armstrong, 26, ambaye anamaliza mwaka wa mwisho wa kandarasi yake katika klabu ya Celtic. (Express)
NeymarHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Real Madrid iko tayari kulipa dau la £307m kuishawishi Paris St-Germain kuondoa kifungu cha kandarasi yake cha kumruhusu mshambuliaji wa Brazil Neymar, 26. kuondoka klabu hiyo. (Sun)
Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte anaonekana kuwa miongoni mwa wakufunzi wanaosakwa na Real Madrid kuchukua mahala pake Zinedine Zidane. (Express)
Kocha wa Chelsea Antonio Conte
Manchester United imehusishwa na uhamisho wa kiungo wa kati wa Brazil Talisca ,24, lakini mchezaji huyo amejiunga na klabu ya China Guangzhou Evergrande kwa mkopo hadi Januari 2019 kutoka Benfica.(Sun)
Klabu mpya katika ligi ya Uingereza iliopandishwa hadhi Wolves huenda ikamsaini kipa wa Ureno mwenye umri wa miaka 30 Rui Patricio, ambaye amevunja mkataba wake katika klabu ya Sporting Lisbon. (Express & Star)
Kocha wa Manchester City Pep GuardiolaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKocha wa Manchester City Pep Guardiola
Beki wa kati wa Uingereza John Stones anasema kuwa mkufunzi wake wa Manchester City Pep Guardiola amemwambia kwamba anaweza kumuandikia ama hata kumpigia simu wakati wowote ule wakati wa kombe la dunia. (Guardian)
Beki wa kushoto wa Southampton Ryan Bertrand anasema kuwa mkufunzi wa Uingereza alikuwa na heshima ya kumpigia simu na kumwambia ni kwa nini hakuorodheshwa katika kikosi cha kombe la dunia -licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kuhisi kwamba bado anafaa kuelekea Urusi. (Mail)

No comments:

Post a Comment