TANGAZO


Sunday, August 25, 2013

Mahafali ya Darasa la Saba, Shule ya Msingi Upanga jijini Dar es Salaam yafana

Wahitimu wa Elimu ya Msingi (Std Vll) 2013 wa Shule ya Msingi Upanga, wakiimba kwaya ya kuwaaga walimu wao pamoja na wanafunzi wenzao, wanaoendelea na masomo yao shuleni hapo wakati wa mahafali yao yaliyofanyika shuleni hapo jana. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Wahitimu wa Elimu ya Msingi (Std Vll) 2013 wa Shule ya Msingi Upanga, wakiimba kwaya ya kuwaaga walimu wao pamoja na wanafunzi wenzao, wanaoendelea na masomo yao shuleni hapo wakati wa mahafali yao hayo jana.
Wahitimu wa Elimu ya Msingi (Std Vll) 2013 wa Shule ya Msingi Upanga, wakiimba mashairi wakati wa wakati wa mahafali yao hayo jana.
Mgeni rasmi katika mahafali ya darasa la Saba ya Shule ya Msingi Upanga, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Wazazi ya shule hiyo, Ally Semsela (kushoto) na Mwalimu Mkuu, Paskazia Kinyondo, wakati wa mahafali hayo jana.
Baadhi ya wazazi na walezi wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Upanga, wakiwa katika mahafali hayo jana.
Wanafunzi wakiigiza kama mgonjwa na daktari wakati wa mahafali yao hayo jana.
Wanafunzi wakicheza ngoma ya Kibati ya wenyeji wa Kisiwa cha Pemba, wakati wa mahafali hayo jana.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika mahafali ya shule hiyo, shuleni hapo jana.
Baadhi ya wahitimu wa Darasa la Saba wakiwa katika mahafali yao hayo jana.
Wanafunzi wa shule hiyo wakicheza ngoma za kitamaduni wakati wakiwaburudisha wageni mbalimbali waliohudhuria mahafali hayo jijini jana.
Baadhi ya walimu wa shule hiyo ya Upanga wakicheza ngoma hizo, sambamba na wanafunzi hao.
Walimu wakizirudi ngoma za kitamaduni wakati wa hafla hiyo jijini jana.
Wanafunzi wa shule hiyo,wakiwa pamoja na baadhi ya wazazi waliohudhuria mahafali hayo jana.
Baadhi ya walimu wa shule hiyo ya Upanga wakicheza ngoma ya Kibati, sambamba na wanafunziwao hao, wakati wa mahafali nayo jana.
Wanafunzi wakizirudi ngoma za kitamaduni wakati wa mahafali hayo hapo jana.
Viongozi Meza Kuu wakifurahia ngoma za kitamaduni zilizokuwa zikipigwa na kuchezwa na wanafunzi wa shule hiyo, wakati wa mahafali hayo jana.
Baadhi ya walimu wa shuleya jirani ya Maktaba wakiwa katika hafla hiyo jana.
Wanafunzi wakionesha mavazi ya Khanga na Kitenge wakati wa mahafali hayo, shule ni hapo jana.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mahafali hayo jana.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ya Msingi ya Upanga, Paskazia Kinyondo, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mahafali hayo jana. 
Wanafunzi, Skauti wa Shule hiyo, wakionesha vipaji vyao, wakati wa mahafali ya shule hiyo jana.
Wanafunzi wakionesha shoo ya kuzirudi ngoma mbalimbali wakati wa hafla hiyo jana.
Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi pamoja na Mkuu wa shule hiyo, Paskazia Kinyondo wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali hayo jana.
Wanafunzi wa shule hiyo, wakizirudi ngoma hizo huku wakitunzwa pesa na wageni mbalimbali waliohudhuria mahafali hayo jana.
Baadhi ya walimu wa shule hiyo, wakiwa kwenye furaha tele wakati wa mahafali hayo jana.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ya Uapnga, Paskazia Kinyondo akisoma risala ya shule hiyo, mbele ya mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (wa pili kushoto), wakati wa hafla hiyo jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wazazi wa shule hiyo, Ally Semsela.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Upanga, Paskazia Kinyondo akikabidhi zawadi Mgeni rasmi, Mkuu wa Wialaya ya Ilala, Raymond Mushji wakati wa mahafali hayo jana.
Mwanafunzi Rukia Jumanne wa darasa la sita, akipokea zawadi yake kutoka kwa Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi kwa kuwa kiongozi bora shuleni hapo, wakati wa mahafali hayo jana.
Irine Joseph wa darasa la Saba, akipokea zawadi yake ya kuwa mwanafunzi Bora mwenye Nidhamu wa shule hiyo.
Eveline Enock akipokea zawadi yake kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi kwa kuwa mwanafunzi Bora anayeongoza kwa usafi shuleni hapo.
Naye Elizabeth Anthony wa darasa la Saba akipokea zawadi yake kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi kwa kuwa mwanafunzi Bora anayeongoza kwa upande wa Taaluma shuleni hapo.
Mwalimu Zainab Mfikilwa, akimpokelea zawadi mwanafunzi wake, Jazil Jamal wa darasa la kwanza wa shule hiyo.
Mwalimu Lilian Kiondo naye amekuwa Mwalimu Bora wa shule hiyo na hivyo naye kukabidhiwa zawadi yake na Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Walimu wakimsindikiza mwalimu Lilian Kiondo (katikati), mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake na Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Walimu wakirudi kwa furaha kumsindikiza mwalimu Lilian Kiondo kuchukua zawadi yake.
Walimu wakirudi kwa furaha kumsindikiza mwalimu Lilian Kiondo.
Mhitimu wa darasa la saba, Kelvi Donald, akikabidhiwa cheti chake cha kuhitimu Elimu ya Msingi na Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Wahitimu wa darasa la saba,wakikabidhiwa vyeti vyao vya kuhitimu Elimu ya Msingi na Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Diwani wa Kata ya Upanga Mashariki, Sultan Salim, akizungumza kabla ya kumnyanyua Mkuu wa Wilaya, Raymond Mushi kuzungumza katika hafla hiyo.
Diwani wa Kata ya Upanga Mashariki, Sultan Salim, naye akipokea zawadi yake katika hafla hiyo.
Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akizungumza wakati wa mahafali hayo jana.
Walimu Tamrina Taalib (kulia) na mwenzake, Mariam Kaposo wakiwa na wanafunzi wao kwenye Klabu yao ya Kujisomea shuleni hapo, wakati wa mahafali hayo jana.
Mwalimu Tamrina Taalib (kulia), akiwaelekeza jambo wanafunzi hao huku mwenzake, Mariam Kaposo (kushoto), akisikiliza kwa makini.
Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ramond Mushi akipatiwa maelezo na Zainab Maneno, kuhusu somo la Sayansi katika topiki ya Polination wakati wa maonesho ya taaluma kwenye mahafali hayo jana.
Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ramond Mushi akipatiwa maelezo na Leila Jamali kuhusu sumaku inavyokubaliana na mwenzake katika poli tofauti na vile vile isivyokubaliana katika poli ya aina moja.

4 comments:

  1. Hi Everyone!
    I'm Elizabeth. I really enjoyed very much with this article here. Really it is an amazing article I had ever read. I hope it will help a lot for all. Thank you so much for this amazing posts and please keep update like this excellent article.thank you for sharing such a great blog with us. expecting for your.

    http://onedaytop.com/smoke-meets-fire-donald-trump-jr-emailed-russia/

    ReplyDelete
  2. Oh my god, mimi ni huyo msichana hapo anaeonesha sumaku na ambae anaongoza kwaya hapo juu kiukweli nimefurahi sana kuona post hizi.

    ReplyDelete
  3. Article ideas very clear . Your writing style is very unique. I very much appreciate the articles you write. Thanks a lot for sharing. Please visit to know
    https://www.lcrenovation.co.uk/loft-conversion-in-battersea/
    House Renovations in Battersea

    ReplyDelete