TANGAZO


Saturday, June 9, 2018

Kwa nini Malkia Elizabeth anasherehekea siku mbili za kuzaliwa

Malkia Elizabeth

Haki miliki ya pichaEUROPEAN PHOTOPRESS AGENCY
Image captionMalkia Elizabeth
Malkia Elizabeth anasherehekea siku ya kuzaliwa kwake ya 92 siku ya Jumamosi ambapo atasherehekea kuongeza miaka yake na mwaka mmoja zaidi.
Alifikia umri wa miaka 92 mnamo mwezi Aprili.
Lakini hatua hii ni kwa sababu Malkia anasherehekea siku mbili za kuzaliwa kila mwaka.
Siku ya kwanza anayosherehekea ambayo ndio aliozaliwa ni ile ya tarehe 21 mwezi Aprili 1926.
Ya pili ni ile inayosherehekewa na umma Jumamosi ya pili mwezi Juni.
Basi kwa nini malkia awe na siku mbili za kuzaliwa na anazisherehekea vipi?.
  • Kwa nini watu wasisherekee siku kamili aliyozaliwa?
Huyu hapa malkia alippkuwa mtoto akibebwa na mamake 1926Haki miliki ya pichaPA
Image captionHuyu hapa malkia alipokuwa mtoto akibebwa na mamake 1926
Awali sherehe rasmi za kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya Mfalme ama hata malkia nchini Uingereza zimefanywa katika siku ambayo sio waliozaliwa.
Utamaduni wa kua na siku mbili za kuzaliwa ulianza yapata miaka 250 iliopita wakati wa Mfalme George wa pili 1748.
Alizaliwa mwezi Novemba ambao haujulikani nchini Uingereza kutokana na hali yake mbaya ya anga.
Lakini mfalme George alitaka siku yake ya kuzaliwa kusherehekewa nchini humo na mwezi Novemba haukuwa mwezi mzuri.
Hivyobasi aliamua kuadhimisha siku hiyo wakati wa sherehe za gwaride la kijeshi la kila mwaka wakati wa majira ya joto- ambapo hali ya anga ni nzuri.
Na hivyo ndivyo utamaduni wa kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mfalme ilipoanza.
  • Anasherehekea vipi siku yake ya kuzaliwa?
Hii ni picha ya mizinga maalum inayopigwa kusherehekea kuzaliwa kwa malkiaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionHii ni picha ya mizinga maalum inayopigwa kusherehekea kuzaliwa kwa malkia
Mara nyingi Malkia husherehekea siku ya kuzaliwa kwake na familia yake ijapokuwa kuna mizinga maalum inayopigwa hewani mjini London mchana kuadhimisha siku hiyo.
Lakini siku yake rasmi ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa huadhimishwa hadharani kupitia kuwepo kwa gwaride kubwa mjini London kwa jina Trooping the Colour.
Gwaride la trooping colours linaloadhimisha siku rasmi ya kuzaliwa kwa malkia ElizabethHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionGwaride la trooping colours linaloadhimisha siku rasmi ya kuzaliwa kwa malkia Elizabeth
Trooping the Colour imeadhimisha siku rasmi ya kuzaliwa ya mfalme wa Uingereza kwa kipindi cha miaka 260 iliopita.
Zaidi ya wanajeshi 1400, farasi 200 na wanamuziki 400 hushiriki katika hafla hiyo , hivyobasi ni tamasha kubwa.

No comments:

Post a Comment