TANGAZO


Saturday, June 9, 2018

Mkutano wa G7 wakumbwa na tofauti kati ya Trump na washirika wake

Rais Trump


Image captionMkutano wa G7 wakumbwa na tofauti kati ya Trump na washirika wake

Mazungumzo katika mkutano wa mataifa yalioendelea kiviwanda dunia G7 yanayofanyika nchini Canada yameshindwa kutatua tofauti kubwa zilizopo kati ya rais wa Marekani Donald Trump na viongozi wa mataifa mengine wanachama.
Tofauti hizo zilizuka hadharani siku ya Ijumaa hususan kuhusu biashara.
Washirika wa Marekani wamekasirishwa na hatua ya rais Trump ya hivi karibuni kutoza ushuru vyuma na bidhaa za aluminium, hatua inayozua hofu ya kuzuka kwa vita vya kibishara.
Haijulikani iwapo makubaliano ya pamoja yatawekwa hadharani baada ya kukamilika kwa mkutano huo baadaye siku ya Jumamosi.
Mkutano huo wa siku mbili unafanyika katika mji wa La Malbaie, mkoani Quebec.
Bwana Trump anatarajia kuondoka siku ya Jumamosi kwa mkutano muhimu na rais wa Korea Kaskazini Kim Jong un.
  • Tofauti ni kubwa zaidi ya biashara
Kulingana na mwandishi wa BBC kuhusu maswala ya kidiplomasia James Robbins, mjini Quebec, mkutano huo ulianza vibaya na unaweza kukamilika bila makubaliano hayo ya pamoja kuafikiwa na wote.
Tofauti kati ya Trump na viongozi wengine sita ni zaidi ya tofauti za kibishara zilizopo- zinashirikisha hali ya tabia nchi, uhusiano na Iran na mgogoro kati ya Israel na Palestina.

Image captionRais Trump akiandamana na waziri mkuu wa Uingereza Theresa May na Kansela wa Ujerumani bi Angela Merkel

Kansela wa Ujerumani Angel Merkel ni ,miongoni mwa wale wanaolalamika kwamba itakuwa vyema kuweka tofauti hizo hadharani badala ya kudanganynaa kuhusu umoja wao.
''Ni uaminifu zaidi'', alisema.'' badala ya kujifanya kwamba kila kitu kiko sawa''. Wengine wanaamini kwamba kunaweza kupatikana kwa maelewano na rais Trump anasema kuwa ana matumaini ya kupata suluhu .
Lakini hakuna tashwishi kuhusu kutengwa kwa bwana Trump.
Hapendi kujadiliana na makundi na ataondoka kabla ya mkutano huo kukamilika akielekea Singapore ili kukutana ana kwa ana na Kim Jong un vile anavyotaka.

Kwa nini kuna tofauti?


Image captionMkutano wa G7 uliopita wakati wa utawala wa rais wa Barrack Obama

Mnamo tarehe mosi mwezi Juni Marekani iliiweka ushuru wa asilimia 25 kwa vyuma na ushuru wa silimia 10 kwa aliminium inayoingia nchini humo kutoka EU, Canada na Mexico .
Bwana Trump alisema kuwa hatua hiyo itawalinda wazalishaji wa nyumbani ambao ni muhimu kwa usalama wa taifa hilo.
Muungano wa Ulaya baadaye ulitangaza kutoza usuru bidhaa zinzotoka Marekani kutoka baiskeli za Harley-Davidson hadi mvinyo wa bourbon.
Canada na Mexico pia zinapanga hatua za kulipiza kisasi.
Siku ya Ijumaa waziri wa maswala ya nchi za kigeni nchini Canada alitaja ushuru huo kama haramu .
Rais wa baraza la Ulaya Donald Tusk amesema kuwa ushuru huo unatishia sheria za kimataifa.
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ameitaka Ulaya kujizuia .Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema kuwa anaamini kwamba pande zote zinataka kuafikia makubaliano.

Image captionNi nani aliyemwachia alama rais Donald Trump katika mkutano wa G7

G7 ni nini?

Ni mkutano wa kila mwaka unaoleta pamoja mataifa ya Canada, Marekani, Uingereza, Ufaransa, Italy, Japan na Germany, ambayo yanawakilisha asilimia 60% ya mapato yote ya kibishara duniani kati yao.
Uchumi ndio ajenda kuu ijapokuwa mkutano huo huangazia maswala muhimu duniani.
Urusi iliondolewa katika mkutano huo 2014 baada ya kuvamia na kuliteka eneo la Crimea kutoka Ukraine.
Siku ya Ijumaa , bwana Trump aliwasilisha ombi lililowashangaza wengi kwa Urusi kurudishwa , lakini kansela wa Ujerumani Angela Merkel alisema kuwa wanachama wengine wanapinga wazo hilo

No comments:

Post a Comment