TANGAZO


Friday, June 8, 2018

Isaya Yunge: Kijana Mtanzania anayetarajiwa kufanikiwa sana katika teknolojia

Isaya Yunge

Isaya Yunge ni miongoni mwa vijana wawili Watanzania wa chini ya miaka 30 wanaotarajiwa na Forbes kuwa mabilionea karibuni.
Yunge ni mwanzilishi wa kampuni ya Soma App, hatua hiyo ni kuondoa shida alizozipitia alipokuwa akitafuta udhamini wa masomo yake ya elimu ya juu.
Nia yake ilikuwa kusaidia vijana wenzake kupitia app ya Soma.
"Nilipomaliza chuo nilitafuta vijana wenzangu wenye akili sana ambao wamesoma Tanzania tukakaa, tukaunda kitu tunaita algorithm ni lugha ambayo hutumika kutengeneza software ambapo kompyuta huwasiliana na kifaa kingine kutoa majibu sawasawa na yalivyoulizwa," ameambia mwandishi wa BBC Leonard Mubali.
Amekuwepo kwenye jarida la Forbes akiorodheshwa kuwa mmoja wa vijana wanaoelekea kuwa na mafanikio makubwa barani Afrika.
Zaidi ya wanafunzi 7000 kutoka barani Afrika wanatumia mtandao wa Soma App uliozinduliwa mwaka 2017.
Forbes imesema Kampuni ya App itakuwa na mafanikio makubwa Afrika siku za usoniHaki miliki ya pichaISAYA YUNGE
Image captionForbes imesema Kampuni ya App itakuwa na mafanikio makubwa Afrika siku za usoni
Mradi huu ulianza na wanafunzi wa kitanzania 550 ambao tayari wamepata ufadhili kutoka Tanzania, Nigeria,Uganda na Rwanda, idadi ambayo inaongezeka.Ufadhilli wa kiasi cha dola 850,000 huzolewa kila mwaka.
''Wanafunzi Afrika hufungua tovuti nyingi zaidi ya 50 kutafuta ufadhili na aweze kupata chuo ambacho kinahitaji mtu mwenye sifa za kufanana naye''.
Soma App imewasaidia wanafunzi zaidi ya 500 nchini Tanzania kupata ufadhili wa masomo nchi mbalimbaliHaki miliki ya pichaISAYA YUNGE
Image captionSoma App imewasaidia wanafunzi zaidi ya 500 nchini Tanzania kupata ufadhili wa masomo nchi mbalimbali
''Soma App inarahisisha zoezi hilo, inamuwezesha mtu kueleza kiwango cha elimu yake kisha kitamsaidia kuuliza kwa sifa hizo atapata chuo kipi kwa kuzingatia sifa za mwombaji..ndani ya muda mfupi majibu yatamfikia yakiorodhesha anafaa kuomba chuo gani kwa kuzingatia sifa hizo''alieleza Yunge.
Forbes imetambua kuwa Soma App itakuwa kampuni kubwa sana Afrika siku za usoni, na inaelezwa kuwa itakuwa na kipato kikubwa, kiasi cha dola milioni mia mbili kwa mwaka.
Ndani ya miaka mitano watakuwa wamekuwa sana Afrika na kufungua matawi mengine katika nchi za Afrika.
Soma App ina wafanyakazi sita kwa sasa na wengine ni wanafunzi wanaofanya kazi kwa vitendo 14 kutoka Mauritius na Rwanda.

No comments:

Post a Comment