TANGAZO


Friday, June 8, 2018

Kwa Picha: Ujenzi wa reli ya kisasa unavyoendelea Tanzania

Wajenzi wakiwa kazini

Image captionWajenzi wakiwa kazini
Nchini Tanzania mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge - unaendelea. Reli hiyo itakayoanzia bandari ya Dar es Salaam hadi mji mkuu wa Dodoma na baadaye hadi nchi za jirani za Rwanda Burundi na DR Congo.
Mradi huo umeelezwa kuwa mkubwa zaidi katika miundombinu kufanyika miaka ya hizi karibuni na manufaa yake kiuchumi kuwa makubwa si kwa Tanzania tu bali hata nchi za jirani.
Waandishi wa BBC Sammy Awami na Nico Mtenga wamekuwa wakifuatilia maendeleo ya mradi huo na waliangazia jinsi mradi huo unavyoendelea eneo la Soga, katika mkoa wa Pwani.
Ujenzi
Mabadiliko haya ni ya kuja kwa reli mpya ya Standard Gauge ambayo si tu itakuwa ya kisasa Nilizungumza na abiria niliowakuta stesheni hapo juu ya matarajio yao
Alitembelea pia ujenzi unaoendelea ambapo wakandarasi walinieleza kuwa wako ndani ya muda.
Awamu ya kwanza yenye umbali wa KM zaidi ya 400 kutoka bandari ya Dar es Salaam hadi Dodoma unatarajiwa kukamilika 2019
Lakini lengo hasa ni kuziunganisha nchi jirani kama Rwanda, Burundi, Uganda na DR Kongo na reli hiyo.
Ujenzi
Ni mradi mkubwa kabisa wa miundo mbinu ambao Rais John Magufuli haachi kuupigia chepuo.
Ujenzi wa reli
"Kwa kutumia reli hii mtu atasafiri kutoka Dar es Salaam hadi hapa Dodoma kwa saa 3 tu ikilinganishwa na saa 5 hadi 6 zinazotumika hivi sasa kusafiri kwa gari, na pia mtu atasafiri kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa saa 9 ikilinganishwa na saa 36 anazotumia sasa kwa kutumia treni," Machi mwaka huu.
Wakati huo alikuwa anaweka jiwe la msingi la kipande cha pili cha mradi wa ujenzi wa reli hiyo kinachoanzia Morogoro hadi Makutupora Mkoani Dodoma.
"Bila shaka hii itaongeza mapato katika bandari yetu ya Dar es Salaam na pia itaimarisha biashara hususani kati ya nchi yetu na nchi zinazohudumiwa na ushoroba wa kati wa nchi za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya kongo (DRC), Rwanda na Uganda."
Ujenzi wa reli
Mradi huo utagharimu dola Bilioni 1.92, lakini ndio utakuwa mradi nafuu zaidi wa reli kufanyika Afrika Mashariki.
Gharama hiyo ni nusu ya ile ambayo Kenya ilitumia kujenga awamu yake ya kwanza ya reli ya hivi karibuni kutoka Mombasa hadi Nairobi.
Reli ya kisasa
Wakati serikali ikisema itagharamia yenyewe kipande cha KM 400 cha mradi huu, wapo wanaopinga mpango huu akiwemo Zitto Kabwe.
Bw Kabwe ni mbunge wa upinzani ambaye ni mmoja wa watu wanaoamini kwamba sekta binafsi ilipaswa kuhusishwa katika ugharamiaji wa mradi huo.
Anasema juhudi zaidi zingeangazia kukarabati mfumo uliopo wa reli kuhakikisha unafanya kazi kwa asilimia 100, na kuutumia "kupata pesa za kujenga reli mpya".
"Kuna miradi ya ukarabati ambayo hufadhiliwa na Benki ya Dunia lakini serikali ilikataa."
Ujenzi wa reli
Treni za mizigo zinatarajiwa kubeba tani milioni 17 za mizigo kwa mwaka.
Hii, si tu itapunguza uharibifu wa barabara kutokana na malori ya mizigo lakini itaongeza pia kasi ya biashara nchini na nchi za jirani pia.
Wachumi na wachambuzi wanaamini uwekezaji huu unaendana na matunda ya kiuchumi ya baadaye.
Mchumi Prof Haji Semboja anasema: "Asilimia zaidi ya 70 ya Watanzania huishi maeneo ya mashambani wakishiriki shughuli za kilimo. Wanahitaji kuunganishwa na masoko ya kitaifa na kimataifa.
MagufuliHaki miliki ya pichaIKULU, TANZANIA
Image captionDkt Magufuli akikagua mfano wa Reli hiyo ya Kisasa mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma Machi mwaka huu.
"Kwa hivyo, umuhimu wa mfumo huu wa reli sio tu kuchochea ustawi maeneo ya mashambani bali pia kusaidia kubadilisha uchumi wa Tanzania."
Nchi kama Ethiopia bado haijanufaika na reli yake mpya kuelekea Djibouti katika kiwango ilichokitarajia wakati wa ujenzi, wengi wanatahadharisha juu ya matarajio ya Tanzania kwamba wakati manufaa ya kiuchumi yanaonekana kuwa wazi hivi sasa, lolote linawezekana.
Kadhalika, kuna uwezekano matunda yasifikie kiwango kinachotarajiwa au yakachelewa kuonekana kinyume cha matarajio ya wengi.

No comments:

Post a Comment