Mwanafunzi Omary Mganga (kushoto), akikabidhiwa cheti
Na Mwandishi wetu
BODI ya Filamu Tanzania leo imemkabidhi cheti na hundi yenye thamani ya shilingi
Laki Mbili mwanafunzi Omary Maganga aliyefanya vizuri kwenye masomo ya filamu
na runinga kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA).
Makabidhiano
hayo yamefanyika kwenye ofisi za bodi hiyo ambapo Afisa Uhusiano na Mawasiliano
Abuu Kimario alimkabidhi cheti hicho na hundi kwa niaba ya Katibu Mtendaji
Joyce fisoo.
Baada
ya kukabidhiwa zawadi zake bwana Maganga aliishukuru Bodi hiyo ya filamu kwa
kutambua juhudi za wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye masomo yao. Pia ameziasa
taasisi zingine za Serikali na zisizo za kiserikali kuwatambua wanafunzi
wanaofanya vizuri kwani kwa kufanya hivyo kunaongeza morali na ushindani.
Wakati
huo Afisa Uhusiano na Mawasiliano Abuu Kimario kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa
bodi hiyo ametoa ahadi ya kuendelea kutoa zawadi kwa wanafunzi wanaofanya
vizuri kwenye masomo yenye uhusiano na tasnia ya filamu.
Kwa sasa Bodi ya
Filamu Tanzania iko kwenye utekelezaji wa programu ya kutambua na kukuza vipaji
vya wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye masomo ya tasnia ya filamu nchini.
Program hii ilianzishwa ikiwa na lengo la kukuza ubora wa filamu za Kitanzania.
No comments:
Post a Comment