Jaji Mkuu wa Australia ya Kusini, Mhe. Christopher Kourakis (kushoto), akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) katika halfla fupi iliyofanyika leo tarehe 7.10 .2016 kwenye ukumbi wa maktaba wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto), akizungumza na Jaji Mkuu wa Australia ya Kusini, Mhe. Christopher Kourakis(katikati) na (kulia) ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania,Bi. Katarina Revocati katika mkutano huo ulifanyika leo tarehe 7.10 .2016 kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Katiba na Sheria uliopo jijini Dar es Salaam.
Jaji Mkuu wa Australia ya Kusini, Mhe. Christopher Kourakis (kulia) akizungumza kuhusu ziara yake ya siku tatu aliyoifanya nchini na kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali ya mafunzo, sheria na shughuli za kimahakama baina ya nchi hizo mbili. (Kushoto) ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe. Mkutano huo ulifanyika leo tarehe 7.10.2016 kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Katiba na Sheria uliopo jijini Dar es Salaam.
Jaji Mkuu wa Australia ya Kusini, Mhe. Christopher Kourakis akiangalia na kupata maelezo juu ya mfumo wa kielektroniki wa kusajili mashauri kutoka kwa Karani wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyopo jijini Dar es Salaam Bw. Abdalla Bugalo wakati alipoitembelea leo tarehe 7.10 .2016. (Picha zote na Mahakama ya Tanzania)
No comments:
Post a Comment