Mawaziri kutoka Mataifa 160 wanakongamana hii leo jijini Nairobi ikiwa siku ya kwanza ya Kongamano la Shirika la Biashara Dunani, WTO.
Ni mkutano wa kwanza ya aina yake barani Afrika.Mjadala mkuu unatarajiwa kuwa mwelekeo mpya kwa mataifa ambayo hayajanawiri, hasa baada ya maafikiano ya Kongamano ka Doha kutotimizwa baada ya zaidi ya miaka kumi.
Zaidi ya wawakilishi 7,000 wanakongamana katika ukumbi wa mikutano ya KICC kuanzia hii keo kujadili jinsi ya kufanya biashara kote ulimwenguni kwa usawa.
Licha ya kuwa bara afrika lina wanachama wengi zaidi katika WTO, kumekuwa na malalamishi kuwa shirika hilo limetawaliwa sana na mataifa yalionawiri tayari, kama Uchina na Marekani.
Bwana Robert Azevedo , ambaye ni mkurugenzi Mkuu wa WTO, umuhimu wa WTO kwa wanachama kutoka afrika.
Naye akasema Afrika inapata Fursa ya kujieleza na kuweka bayana matakwa yake kibiashara. ''Afrika inapewa Meza ya kusema matarajio yake,
Mahala pa kuketi.
Kipaza sauti ya kusema nacho. Mataifa haya hayezi kupuuzwa.
Hayawezi kusahaulika.
Na hali hii huenda likatimika ikiwa WTO haitendi kazi yake vizuri, au haizingatii maswala yote muhimu, kama vile biashara ndogo ndogo na zile wastani, na vile zitawiana na msururu wa biashara za kimataifa.
Ni jinsi gani ya kusaidia mataifa ya Afrika kunawiri kiviwanda?
Njia bora zaidi ni kuyapa mataifa jukwaa ya kushiriki, kutoa maoni, na kusema ni njia gani tuwaweza kuwasaidia.''Alisema Azevedo
Kwa zaidi ya miaka ishirini shirika la WTO imefanya majadiliano bila kuafikiana jinsi mataifa masikini yatasaidiwa kufanya biashara.
Kwenye Kongamano la Doha ya Mwaka 2001, mataifa masikini yaliomba ruzuku katika biashara za sekta ya Kilimo wanayotegemea sana bila mafanikio.
Mataifa mengi sasa yanafanya makubaliano ya makundi madogo, kwa mfano jumuiya ya Afrika Mashariki au Muungano wa Kenya, Uganda na Rwanda, ambao umerahisisha usafiri wa raia wa nchi hizo pamoja na bidhaa kutoka bandari ya Mombasa.
Bw Azevedo anasema ni wakati wa WTO kuinuka sambamba na miungano kama hii.
Azevedo''Na hii ndio sababu kongamano la Nairobi ni muhimu sana. Ni wakati wa kutafakari, Nadhani wanachama watazungumza na kujadili maswala haya nyeti kama mawaziri, kwa hivyo ni mjadala muhimu kisiasa''
Azevedo hatarajii makubaliani katika maswala yote tata, ila ana matumaini kuwa mjadala utazua angalau msimamo mmoja kuhusu mwelekeo wa pamoja wa siku za usoni.
Kati ya mataifa arobaini na tatu kutoka Afrika ambayo ni washiriki wa WTO, 33 zinatambulika kama mataifa masikini, ikiwemo Tanzania, Uganda na Sudan Kusini.
Ethopia haijajiunga na WTO ingawa imewasilisha ombi. Katika kongamano la mwaka huu wanachama watapiga kura kuamua ikiwa mataifa ya Liberia na Afghanistan watakubaliwa kuwa wanachama.
Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf yuko Kenya kushuhudia uamuzi huo.
No comments:
Post a Comment