Saudi Arabia imetangaza kuunda muungano mpya wa kijeshi wa nchi 34 za kiislamu wa kukabiliana na ugaidi.
Shirika rasmi la habari la Saudi Arabia limesema kazi ya muungano huo itaratibiwa katika kituo cha pamoja mjini Riyadh.
Wajumbe wa muungano huo ni mataifa ya kiarabu, Afrika na Asia Kusini .
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, waziri wa ulinzi wa Saudia , Mwanamfalme Mohammed bin Salman, amesema kua muungano huo utaratibu juhudi za mapigano dhidi ya makundi yenye itikadi kali katika mataifa ya Syria, Iraq, Libya, Misri na Afghanstan .
Hata hivyo kuna taarifa chache kuhusu namna kikosi hiki kitakavyotekeleza majukumu yake.
Mataifa ya ghuba yanakabiliwa na shinikizo kufanya juhudi zaidi katika vita dhidi ya kundi la Islamic State nchini Iraq na Syria
Oroda ya mataifa katika muungano huo
- Saudi Arabia,
- Bahrain,
- Bangladesh,
- Benin, Chad,
- Comoros,
- Djibouti,
- Misri,
- Gabon,
- Guinea,
- Ivory Coast,
- Jordan,
- Kuwait,
- Lebanon,
- Libya,
- Malaysia,
- Maldives,
- Mali,
- Morocco,
- Mauritania,
- Niger,
- Nigeria,
- Pakistan,
- Palestina,
- Qatar,
- Senegal,
- Sierra Leone,
- Somalia,
- Sudan,
- Togo,
- Tunisia,
- Uturuki,
- Milki za Kiarabu
- Yemen.
No comments:
Post a Comment