TANGAZO


Tuesday, December 15, 2015

Kerry na Putin kujadiliana kuhusu Syria

Urusi
Marekani imetofautiana na Urusi kuhusu makundi ya wapiganaji Syria

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani John Kerry yumo nchini Moscow kwa mashauriano na Rais Vladimir Putin kuhusu njia za kumaliza vita Syria.

Mazungumzo hayo yanalenga kupunguza ufa kati ya Urusi na Marekani, hasa kuhusu makundi ambayo yanafaa kujuishwa kwenye mazungumzo.

Urusi, ambayo inamuunga mkono Rais wa Syria Bashar al-Assad, imesema mkutano wa majuzi wa makundi yanayopinga serikali ya Syria haukuwakilisha makundi yote.

Aidha, Moscow imesema mkutano huo ulijumuisha ‘makundi ya kigaidi’.
Mwandishi wa BBC mjini Moscow anasema licha ya tofauti kubwa kati ya Urusi na Marekani, Bw Kerry ataweka msingi kwa mazungumzo kati ya mataifa yenye ushawishi duniani kuhusu mzozo huo wa Syria baadaye wiki hii mjini New York.

Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria yamedumu kwa miaka minne sasa.

No comments:

Post a Comment