TANGAZO


Tuesday, March 17, 2015

Kinana aisambaratisha Chadema Karatu, akemea ufisadi uliokithiri

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye ambaye ameambatana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana katika ziara ya Mkoa wa Arusha, akihutubia jioni ya leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Karatu. (Picha zote na Kamanda Richard Mwaikednda wa Kamanda wa Matukio Blog)

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Karatu jioni ya leo, ambapo aliwasihi wananchi wa wilaya hiyo ambayo inaoongozwa na Chadema, kuachana nacho kwani kwa muda wa miaka kumi na mitano iliyoongoza hakuna maendeleo yoyote waliyowaletea zaidi kutumia ovyo fedha zinazopekwa na Serikali wilayani humo kwa ajili ya miradi ya maendeleo.Halmashauri ya Wilaya hiyo inaoongwa na Chadema.
Kinana ambaye yupo mkoani Arusha kwa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi, alishuhudia Halmashauri ya Karatu inayoongozwa na Chadema imekataa kutoa sh. mil 60 zilizotolewa na Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Baray Mbuga Nyekundu, kisa Kata hiyo inaongozwa na Diwani wa CCM.
Nape akihutubia katika mkutano huo uliofurika watu kwenye Uwanja wa Mazingira mjini Karatu.
Wananchi wakishangilia wakati wa mapokezi ya Komredi Kinana alipowasili Wilaya ya Karatu akitokea Wilaya ya Ngorongoro.
Wananchi wakishangilia wakati wa mapokezi ya Komredi Kinana alipowasili Wilaya ya Karatu akitokea Wilaya ya Ngorongoro.
Wananchi wakimshangilia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipokuwa akihutubia katika Kata ya Baray, ambapo Komrdi Kinana alishiriki ujenzi wa Kituo cha Afya cha Baray, ambacho fedha zilizotengwa na Serikali Kuu sh. mil 60 kwa ajili ya ujenzi huo zilizuiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Karatu inaoongozwa na Chadema kwa madai kwamba Kata hiyo inaoongozwa na CCM.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia baada ya kushiriki ujenzi wa Jengo la Upasuaji ala kituo cha Afya cha Baray, ambapo alikemea kitendo cha Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu kuzuia sh. mil. 60 zilizotolewa na Serikali Kuu za ujenzi wa jengo hilo na kuwataka waache kabisa tabia hiyo.
Komredi Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la upasuaji katika Kituo cha Afya cha Baray.
Komredi Kinana akivuka kwenye kidaraja alipokuwa akienda kukagua mfereji wa umwagiliaji mashamba ya vitunguu na kushiriki kupanda zao hilo katika Kata ya Mang'ola, wilayani Karatu.
Kinana akishiriki kupanda zao la vitunguu katika mashamba ya Mang'ola.Mango'ola inaongoza kwa uzalishaji wa vitunguu vizuri Afrika Mashariki na Kati.
Kinana na viongozi wengine wa chama na Seriksli wakielekea kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Mang'ola.
Komredi Kinana akihutubia katika mkutano huo uliofanyika katika Kata ya Mang'ola, inayoongozwa na Chadema, ambapo wananchi wa eneo hilo walimuomba awatatulie matatizo mbalimbali yanayowakabili ambayo kwa asilimia kubwa yamesababishwa na uongozi wa Chadema.

Wananchi wakimkaribisha Komredi Kinana kushiriki ujenzi wa jengo la CCM, Tawi Kilimatembo, wilayani Karatu.
Komredi Kinana akiteremka kwenye ngazi baada ya kushiriki ujenzi wa jengo la tawi hilo.

Komredi Kinana akitoka kukagua jengo la Serikali ya Kijiji cha Kilimatembo Kata ya Rhotia, wilayani Karatu.
Wananchi wakimkaribisha Komredi Kinana kwa shangwe alipofika kufungua rasmi jengo la CCM Tawi la Rhotia. 
Komredi Kinana akihutubia wananchi baada ya kufungua rasmi jengo la kitegauchumi la CCM Tawi la Rhotia.

Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Mazingira mjini Karatu.
Vijana wa Green Guard wa CCM, wakijadiliana jambo walipokuwa wakingalia kwenye simu picha zilizopigwa wakati wa mkutano huo wa hadhara.
Sehemu ya umati wa watu katika mkutano huo.
 Mmoja wa wanachama wapya wa CCM walioihama Chadema, akielezea jinsi chama hicho kilivyowatesa kwa takribani miaka mitano kwa kutowaletea maendeleo.

No comments:

Post a Comment