Waziri wa
Maji Profesa Jumanne Maghembe akiakata
utepe kuashiria uzinduzi wa Maadhimisho ya 27 ya Wiki ya Maji Kitaifa yanayofanyika
katika mji wa Musoma mkoani Mara.
Waziri wa
Maji Profesa Jumanne Maghembe, akisaini
kitabu cha wageni kwenye banda la Idara ya Maji Vijiji iliyoko Wizara ya Maji
wakati akikagua mabanda ya maonesho kwenye shule ya Msingi Mkendo mjini Musoma
mkoani Mara.
Mkemia wa Wizara ya Maji Rocho Mkole akitoa maelezo
kwa Waziri wa Maji Prof. Maghembe wakati alipotembelea banda la wizara hiyo.
Mhandisi wa
Mazingira wa Idara ya Rasilimaji za Maji kutoka Wizara ya Maji, Eng. Modest
Zakari akitoa maelezo kwa Waziri Profesa Maghembe kuhusu kilimo cha umwagiliaji.
Waziri wa
Maji Profesa Jumanne Maghembe akiangalia kifaa cha kupimia maji kwenye banda ya
kampuni ya kampuni ya NFOSYS PS, huku Msambazaji Mkuu wa Wizara Crepi Bulamu na
wataalamu wa kampuni hiyo na wakishuhudia.
Waziri wa
Maji Profesa Maghembe akiangalia baadhi ya mitambo ya banda la kampuni ya DPI
Simba Limited wakatia akitembelea mabanda.Kulia ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo
Jai Patidar.
Waziri Profesa Maghembe (katikati) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Mara Kapteni
Mstaafu Aseri Msangi.Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mbogo
Futakamba.
Waziri wa Maji Prof. Maghembe akihutubia wananachi.
Waziri wa
Maji Profesa Maghembe, akizungumza na wanahabari.
Kikundi cha burudani kikiburudisha, wakati wa hafla hiyo.
Mwalimu
Msomi wa Shule ya Sekondari Kisangula kutoka Wilaya ya Serengeti, akiongoza
wimbo wa kuhamasisha kutunza vya nzo vya maji.
Mkuu wa
Idara ya Rasilimali za Maji na Uhandisi wa Umwagiliaji wa Chuo cha Maji, Eng.
Pantaleo Tumbo akitoa elimu kwa wananchi waliohudhuria kwenye maonesho ya
maadhimisho ya wiki ya maji. (Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO)
Na Hussein
Makame-MAELEZO
ZAIDI ya
wananchi Milioni 7 wamepatiwa maji safi na salama katika miji ya mikoa, wilaya
na miji midogo nchini kutokana na kuboresha huduma za majisafi na uondoaji
majitaka mijini.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Maji, Profesa Jumanne
Maghembe wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Maji Kitaifa
yanayofanyika katika shule
ya Msingi Mkendo mjini Musoma mkoani Mara.
Prof.
Maghembe amesema uboreshaji huo ni kujenga, kukarabati na kupanua miundombinu
ya majisafi katika miji mikuu ya mikoa, wilaya, miji midogo na miradi ya maji
ya kitaifa.
AlisemaSerikali
kupitia Programu ya Maendeleo ya Sekta
ya Maji imejenga miradi mipya 663 imejengwa katika vijiji 10 kwa kila
halmashauri nchini na miradi 68 ya upanuzi na ukarabati kupitia Mpango wa Matokeo
Makubwa Sasa (BRN).
“Utekelezaji
huo umekamilisha miradi 731 iliyopangwa kutekelezwa na unajumuisha miradi 390 ambayo
haikukamilika katika mwaka wa fedha 2013/2014” alisema Prof. Maghembe na
kuongeza:
“Kuanzia
mwezi Julai 2013 hadi mwezi Desemba 2014, jmla ya miradi ya maji 674 ilijengwa
na kukamilika.Idadi hii inatokana na ujezni wa miradi mipya 433 ya vijiji 10
katika kila halmashauri na miradi mingine 241 ya upanuzi na ukarabati”.
Alifafanua
kuwa miradi hiyo imevipatia maji vijiji 900 na jumla ya vituo vya kuchotea maji
18610 vilivyojengwa ambavyo vinahudumia watu 4,568,402 na kuanzisha vyombo vya
watumia maji 560.
“Usimamizi
huo imepelekea kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama
vijijini kutoka asilimia 40 Julai 2013 hadi asilimia 53.08 za sasa” alisema
Profesa Maghembe.
Kwa upande
wake Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kapteni Mstaafu Aseri Msangi aliwataka wananchi
kutunza vyanzo vya maji ili kuhakikisha kuwa wanapata maji kwa muda wote.
Alikizungumzia
hali ya maji Kapteni Mstaafu Msangi alisema kwa sasa upatikanaji wa maji
vijijini ni asilimia 46.3 wakati maeneo ya mijini upatikanaji wa maji ni
asilimia 53.5.
Naye Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mbogo Futakamba
aliwaasa wananchi, mashirika na wadau wote wa sekta ya maji kuunga mkono jhudi
za kuboresha huduma za maji hapa nchini.
Alisema
lengo la maadhimisho hayo ni kuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi watambue
kuwa maji ni rasilimali muhimu katika kupiga vita umasikini na kuleta maendeleo
ya kiuchumi kwa wananchi.
Waziri Prof.
Maghembe alisema Madhumuni ya Maadhimisho ya Wiki ya Maji ni kuhamasisha, kutoa elimu kwa umma kuhusu
Sekta ya Maji na kusisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki katika mipango ya
utunzaji wa rasilimali za maji na uhifadhi wa mazingira.
Maadhimisho
ya 27 ya Wiki ya Majiyamebeba Kaulimbiu isemayo “Maji kwa Maendeleo Endelevu”
ambapo yataambatana na uzinduzi au uwekaji mawe ya msingi ya miradi ya maji
ikiwemo mradi mkubwa wa Maji wa mji wa Musoma.
No comments:
Post a Comment