Waziri wa Nishati na Madini, Sosperter Muhongo
Na Frankius Cleophace, Tarime.
WAZIRI wa Nishati na Madini Sosperter Muhongo ametembelea Miradi wa umeme Vijijini kwa lengo la kuongea na wananchi huku akikagua miradi hiyo na kutoa kauli mbalimbali za kumalizika mapema kwa zoezi hilo ili wananchi waanze uzalishaji mapema kwa lengo la kusukuma gurudumu la Maendeleo.
Aidha Muhongo alisema kuwa Serikali imeamua kupeleka umeme vijijini kwa lengo la kufuta umaskini ikiwa ni pamoja na kuboeresha sekta ya Elimu.
“Sasa hivi tunajenga maabara zinahitaji umeme na vijiji kama hakuna umeme utategemea watoto kushinda kweli. alisema Muhongo.
Hussein Ayubu ni Injinia kutoka kampuni ya Derm Helecticet (LTD) ifikapo Aprili Mwaka Kesho Vijiji 27 ambavyo vimetengwa katika wilaya ya Tarime vitakuwa vimeanza kutumia Umeme.
“Mh Waziri wa Nishati na Madini ifikapo Aprili 15 wananchi wa kijiji cha Surubu Kata ya Komaswa watakuwa na Umeme” alisema Hussein.
Kwa Upande wake Gissima Nyamohanga ambaye ni Meneja utaalamu Elekezi wakala wa Nishati Vijijini (REA) alisema kuwa kati ya mikoa yote 25 Tanzania Bara vimetengwa Vijiji 1500 kwa ajili ya kupata Umeme huku vikitengewa Billioni Mianane Themanini na Moja ukiwemo mkoa wa Mara ambao umetengewa Billioni 49 kwa ajili ya vijiji 197 chini ya mpango huo wa awamu ya pili.
“Katika wilaya ya Musoma mjini na Vijijini vijiji45 Bunda vijiji45, Rorya Vijiji39, Serengeti vijiji44 na Tarime vijiji24 vyote vitapatiwa umeme kwa awamu hii ya pili ambapo vimetengewa Billioni 49” alisema Muhandisi.
Naye Meneja kanda ya Ziwa Bi: Joyce Ngahyoma akatota angalizo kwa wananchi kuwa wakati huu wa kupitiwa umeme wananchi watalipa shilingi Elfu Ishirini na Saba tu.
“Asije akajitokeza mtu yeyote akawaibia nyie wananchi tutakuwa na mafundi wetu majina ya mafundi yote tayari yapo katika ofisi za mameneja wilaya na Mkoa tutawapeni” alisema Meneja Tanesco kanda yaziwa.
No comments:
Post a Comment