TANGAZO


Saturday, November 8, 2014

Taasisi ya Starkey Hearing Foundation yasaidia wananchi vifaa vya kuongeza usikivu

TAASISI ya Starkey Hearing Foundatioin ikitoa huduma ya kliniki kwa kuwawekea vifaa vya kuongeza usikivu masikioni kwa watu zaidi ya 1000 wenye matatizo ya kusikia katika Mkoa wa Kilimanjaro shughuli iliyoanza jana kwenye viwanja vya Shree Hindu Mandal vilivyopo kando ya barabara ya Mawenzi mjini  Moshi .
Mwanzilishi wa taasisi hiyo, Bill Austin na mkewe Tani wamekuwa wakiongoza zoezi hilo toka lilipoanza majira ya saa mbili asubuhimjini Moshi jana.

Wasichana ambao ni marafiki Lina John ambaye ni albino pamoja na Esther Urassa kutoka Shule Maalumya Mtakatifu Francis iliyopo katika Manispaa ya Moshi walikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa wanatoa msaadakwa watu waliokuwa wanapewa huduma ya kuwekewa vifaa maalum.

 ESTHER Urassa ambaye naye ana tatizo la kusikia akipewa huduma hiyo kabla ya kuwasaidia wenzie.

Lina :  Lina John ambaye ni kipofu akipima kiwango cha sauti kwenye kidevu chake ili kama mtoto Ronald anaweza kusikia mara baada ya kuwekewa kifaa cha kuongeza usikivu:
 Mtaalamu wa masuala ya usikivu na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Starkey Hearing Foundation, Bill Austin, akimhudumia kijana mwenye matatizo ya kusikia Consolata Philemon, kumuwekea vifaa maalum vya kumuongezea usikivu, jijini Arusha leo. 
Derek akiwachunguza wanafunzi wa Msandaka Primary School kabla ya kuwawekea vifaa hivyo wa usikivu.
Fadhili Athuman akichunguzwa kabla ya kuwekewa vifaa vya kuongeza usikivu.
Vijana wakifurahia baada ya kuapatiwa huduma ya vifaa vya usikivu na Taasisi ya Starkey.
Mtoto akijiangalia baada ya kufungwa vifaa vya kumuongezea usikivu.
Watoto wakifahamishwa namna ya kuunganisha betri ya kifaa hicho cha usikivu.
 Hussein Athman akimsaidia Victoria Emmanuel kufunga kifaa hicho.
 Mtaalamu Lina akipima sauti ya kijana baada ya kufungwa kifaa maalum cha usikivu.
 Lina John (kipofu) na Esther Urassa akiwasadia wanafunzi wa St. Francis kuwaweka vifaa hivyo.
 Lina na Esther wakiwa na wanafunzi wao wa St. Francis baada ya kupatiwa huduma hiyo.
 Wakionesha alama ya upendo wakati wa huduma hiyo.
 Vijana wakipatiwa maelezo namna ya kutumia vifaa vya kuongeza usikivu.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Montage wakijitolea kutoa huduma hiyo.
 Vijana wakielekezwa namna ya kuvaa vifaa hivyo.
Paulina Paul akifungwa kifaa cha kuongeza usikivu na Bill Austin.
Lina (mwenye upofu wa macho), akipigwa picha. 
Salim Bakari wa Uhuru Primary School, akifungwa kifaa hicho maalum cha kuongeza usikivu.
 Shani Mohamed akijiangalia kama amevaa vyema.
 Sia Ramadhani akijifunza kurekebisha kifaa cha masikio.
Mtaalamu Stuart Johnson, akiwa kazini kuwaweka vijana vifaa hivyo.
 Wananchi wakisubiri kupatiwa huduma hiyo.
 Tani Austin akimhudumia mgonjwa.
 Kijana akifanyiwa uchunguzi.
 Kijana akifahamishwa jinsi ya kupachika betri katika kifaa hicho.
 Victoria Emmanuel akijiangalia kwenye kioo kama kweli kumempendeza kifaa hicho.
 Wafanyakazi wa Kampuni ya Montage wakijitolea kutoa huduma.
 Wananchi wakisubiri kupatiwa huduma hiyo bure.
Wananchi wakingojea vifaa vya usikivu na kurejesha usikivu kwenye masikio..
 Vijana wakionesha medali zao baada ya kupata huduma ya usikivu bure.
 Vijana wakisalimiana baada ya kupatiwa huduma hiyo.
 Vijana wakiwa wamejipanga mstari wakisubiri huduma hiyo.
Vijana wakiwa wameshikana mikono wakati wa kutolewa huduma hiyo.
Wazee waliopata vifaa hivyo, wakipata ushauri wa kutunza vifaa.

No comments:

Post a Comment