Viongozi wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema Bawacha) wakiwa kwenye kaburi la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, baada ya kuweka mashada ya maua kwenye kaburi hilo jana. (Picha
na Frankius Cleophace)
Na Frankius Cleophace, Butiama
Serikali imetakiwa kutunza makumbusho
ya Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere ili yaendelee kuwepo kwa lengo
la kizazi kijapo.
Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Katibu Mkuu Balaza la wanawake Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Kunti Yusuph kwenye ziara ya kutembelea makumbusho ya Baba wa Taifa katika
kijiji cha Mwitongo wilayani Butiama.
Naibu hiyo alisema kuwa serikali
nimekuwa ikitumia fedha nyingi lakini imesahau kutuna makumbusho ya baba wa
taifa katika hadhi ya kimataifa
“Tumetembelea makumbusho ya Baba wetu
wa taifa lakini huwezi kuyathaminisha na
yale alikuwa akiyafanya hayati Julius Kambalage” aalisema Naibu.
Naye mbunge wa viti maalumu jimbo la
Tarime Mkoania Mara Ester Matiko amezidi kulaani vitendo vya vifo kwa akina
mama nakuwataka kuungana pamoja ili kutokomeza vifo hivyo.
“Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na
usalama ni Mwanamke lakini tunaendelea
kufaliki tunaomba jeshi la polisi kujipanga sawa na si kuja kurekodi
mikutano ya Chadema na kushindwa kusaka waoua” alisema Matiko.
Kwa upande wake mbunge wa viti
maalumu Grace kiwelu aliwataka wananchi kuondokana na ukabira,pamoja na udini ili kudumisha Amani, Upendo na
Mshikamano.
Katika uhai wa hayati Nyerere
alipinga sana ukabira iweje kwa sasa chama cha CCM kishindwe kutetea yale
aliyoyaacha Baba wa Taifa.
Hata Mmoja wa kutunza makumbusho hayoBaraka
Bwire katika kutoa historia ya Hayati lasema kuwa wanakabiliwa na ukosefu wa
fedha ili kuendeleza makumbusho hayo.
“Ruzuku zinatengwa kutoka serikalini
lakini zinafika zikiwa zimechelewa na wakati mwingine ufika kidogo na
kusababisha ukosefu wa fedha zaq kuendeshea na kuboresha makumbusho haya” alisema Bwire.
No comments:
Post a Comment