Rais wa Bunge la SADC ambaye pia ndiye Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda.
Na Owen Mwandumbya, Lusaka Zambia
RAIS
wa Bunge la SADC ambaye pia ndiye Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Anne Makinda kesho tarehe 10 Novemba, 2014 ataongoza ujumbe wa Bunge la
SADC kushiriki Misa Maalum ya kuombea mwili wa aliyekuwa Rais wa Zambia marehemu
Michael Chilufya Sata katika misa maalum itakayofanyika katika viwanja vya Makumbusho
Mjini Lusaka, Zambia.
Katika
ujumbe huo wa Bunge la SADC, Makinda ataongozana na viongozi wengine wa Bunge
hilo ambao ni Spika wa Zimbabwe Mhe. Jaji Jacob Mudenda, Spika wa Bunge la
Afrika Kusini Mhe. Baleka Mbete, Spika wa Bunge la Malawi Mhe. Richard Msowoya Spika
wa Bunge la Angola Mhe. Fernando da Piedade Dias dos Santos na Mwenyeji
wao Spika wa Zambia Dkt. Patrick Matibini.
Kutoka
secretariat ya makao makuu wa Bunge hilo, katibu Mkuu wa Bunge Bunge la SADC
Dkt. Essau Chiviya ataambatana na ujumbe huo kuwakilisha sekretariati ya Bunge
hilo katika Misa hiyo Maalum Mjini Lusaka, Zambia.
Kwa
mujibu wa ratiba ya awali iliyotolewa na Serikali ya Zambia, Misa hiyo Maalum
ya kuombea mwili wa Rais Rata itanyika kesho tarehe 10 Novemba, 2014 na
inatarajiwa kuhudhuriwa na Marais kutoka kila kona ya dunia pamoja na viongozi
mbalimbali wa Kimataifa watakaoziwakilisha nchi zao kabla ya kufanyika kwa mazishi
yake ambayo yamepangwa kufanyika siku ya jumatatu tarehe 11 Novemba, 2014 mjini
Lusaka.
Sata
aliyekuwa na umri wa miaka 77 alifariki tarehe 29 Oktoba, 2014 jijini Londo Uingereza alikokuwa akipatiwa
matibabu ambapo kifo chake kilitokea siku chache baada ya Zambia kusherehekea
miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo, sherehe ambazo hakuweza kushiriki kutokana na
maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.
Mwanasiasa
huyo mkongwe aliingia madarakani mwezi Septemba 2011 baada ya kuongoza chama
chake cha Patriotic Front, na kumshinda Rupiah Banda, ambaye alikuwa rais
wakati huo na chama chake cha Movement for Multi-Party Democracy, kikiwa
madarakani kwa miaka ishirini.
Sata
ambaye alibatizwa jina la "King Cobra" na wafuasi wake wakati alipochaguliwa
mwaka 2011, alionekana kama mbadala wa siasa za Zambia na mtu ambaye alikuwa
wavitendo licha ya kukosolewa kwa sehemu kubwa na upinzania.
Makinda
na ujumbe wake wanatarajia kurudi nchi siku ya jumatano baada kushiriki pia
mazishi yatakayofanyika tarehe 11 Novemba, 2014.
No comments:
Post a Comment