TANGAZO


Sunday, October 12, 2014

Wiki ya Vijana yaendelea kuwa Chachu ya Uzalendo

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiangalia Jarida katika banda la Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Dunia (UNFPA – Tanzania) alipotembelea katika Maonyesho ya Wiki ya Vijana leo mjini Tabora. Kutoka kushoto ni Mchambuzi wa Miradi ya Vijana na Maendeleo wa UNFPA - Tanzania Bi. Tausi Hassan na Mshauri wa Vijana wa Shirika hilo Bw. John Kalimbwabo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwezeshaji Vijana, Jinsia, Wanawake na Watoto ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Ally Hamis akonyesha nyaraka za vibali na sahihi za Wakuu wa Mikoa alipopita Kijana mzalendo Bw.Abiudi Denis aliyetembea nchini nzima kwa Siku 65 kwa lengo la kuhamasisha uzalendo ikwemo kupinga Muundo wa Serikali Tatu, Kumpongeza Rais Jakaya Kikwete na Kupinga watu wanaombeza Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere leo mjini Tabora wakati alipokea Bendera ya Taifa kutoka kwa kijana huyo kwenye Viwanja vya Maonyesho ya Wiki ya Vijana.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel  akitembelea mabanda wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Vijana yanayoendelea katika Viwanja vya Ali Hassan Mwinyi, mkoani Tabora.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwezeshaji Vijana, Jinsia, Wanawake na Watoto ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Ally Hamis (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kijana mzalendo Bw. Abiud Denis (mwenye bendera) aliyetembe nchini nzima kwa Siku 65 kwa lengo la kuhamasisha uzalendo ikwemo kupinga Muundo wa Serikali Tatu, Kumpongeza Rais Jakaya Kikwete na Kupinga watu wanaombeza Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere leo mjini Tabora wakati alipokea Bendera ya Taifa kutoka kwa kijana huyo kwenye Viwanja vya Maonyesho ya Wiki ya Vijana. (Picha zote na Frank Shija, WHVUM)

No comments:

Post a Comment