TANGAZO


Sunday, October 12, 2014

Taifa Stars yapata baraka za viongozi wa Dini

*Yaifumua Benin mabao 4-1
Mchungaji Richard Kamenya wa timu ya Mshikamano, akijitayarisha kumpiga kanzu golikipa Sheikh Muharami Pembe wa timu ya Amani, wakati wa mchezo wa kirafiki wa viongozi wa dini, ulifanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Amani ilishinda bao 1-0 katika mchezo huo. Kushoto ni Sheikh Khamis Mtonga wa Amani. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mchungaji Christilla Kalata wa timu ya Mshikamano, akiumiliki mpira huku akifuatwa na Sheikh Seif Sadiki wa Amani, wakati wa mchezo huo wa utangulizi kabla ya Taifa Stars kumenyana na Benini katika mchezo wa Kirafiki wa Kimataifa, uliochezwa uwanjani hapo leo.
Sheikh Saleh Omar wa Mshikamano (kulia), akiwania mpira na Ustaadh Jawad Idd wa timu ya Aamani.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mchungaji George Fupe, wakati alipokuwa akisalimiana na wachezaji wa timu za viongozi wa dini za Amani na Mshikamano, wakati wa mchezo huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Amani, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akimkabidhi Nahodha wa timu ya Amani, Sheikh Alhad Mussa Salum, kombe la ushindi baada ya timu hiyo, kuifunga Mshikamano bao 1-0, katika mchezo huo wa utangulizi.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi nahodha wa timu ya Mshikamano baada ya kufanikiwa kuwa washindi wa Pili katika mchezo wa viongozi wa Dini uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Stars ilishinda mabao 4-1. 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wachezaji wa timu ya viongozi wa Dini mara baada ya kumalizika mchezo kati ya timu hizo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Upatanishi, Sheikh Mkuu, Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum na wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki. 
Wachezaji wa Stars wakipongezana baada ya kufanikiwa kufunga bao la Tatu katika mchezo wa Kirafiki wa Kimataifa, uliofanyika wanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Hadi katika dakika ya 87, Stars ilikuwa mbele kwa mabao 4-0 kama inavyoonesha kwenye ubao wa matangazo wa uwanja huo.
Mchezaji Salum Aboubakari, akiwania mpira na Badaru Nana wa Benin katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaamjana. Stars ilishinda mabao 4-1.
Thomas Ulimwengu wa Stars, akimtoka Badaru Nana wa Togo wakati wa mchezo huo.
Shomari Kapombe wa Taifa Stars, akikimbia na mpira kuelekea kwenye lango la timu ya Benin, wakati wa mchezo huo. 
Mchezaji Salum Aboubakari, akiwania mpira na Badaru Nana wa Benin katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaamjana. Stars ilishinda mabao 4-1. 
Mchezaji Haruna Chanongo wa Taifa Stars, akikimbia na mpira huku akifukuzwa na Sosa Didier wa Benin, wakati wa mchezo wa Kirafiki wa Kimataifa uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Stars ilishinda mabao 4-1. 
Mchezaji Salum Aboubakari, akiwania mpira na Badaru Nana wa Benin katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Stars ilishinda mabao 4-1.)
Hadi ilipofika dakika ya 88 ndipo Benin ilipopata bao lakufutia machozi na ubao wa matangazo kusomeka Tanzania mabao 4, Benini 1. 
Mashabiki wa Stars wakionesha kufurahishwa na matokeo hao.
Wachezaji wa Stars wakishagilia moja ya mabao ya yaliyofungwa na timu hiyo wakati wa mchezo huo.
Wachezaji wa Stars wakishagilia moja ya mabao ya yaliyofungwa na timu hiyo wakati wa mchezo huo.
Mchezaji Salum Aboubakari, akiwania mpira na Badaru Nana wa Benin katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Stars ilishinda mabao 4-1. 

No comments:

Post a Comment