TANGAZO


Thursday, October 9, 2014

Wakala Huduma za Misitu Tanzania (TFS), yawataka wananchi kufuga nyuki

Ofisa Ufugaji Nyuki Mwandamizi toka wakala wa  Huduma  Misitu Tanzania (TFS), Bw. Steven Msemo (katikati), akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu faida za kufuga nyuki ikiwemo kuongeza kipato cha wananchi  kwa kuuza asali watakayozalisha. Kulia ni Msaidizi wa Misitu Bi Magori Nyancheri  na Kushoto Afisa Habari wa wakala huo Bi. Glory Mziray.
Ofisa Ufugaji Nyuki Mwandamizi toka wakala wa  Huduma  Misitu Tanzania (TFS), Bw. Steven Msemo akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Kongamano la ufugaji Nyuki Afrika litakalofanyika Arusha kuanzia tarehe 11-16 Novemba 2014 ikiwa ni moja ya mbinu za kuboresha ufugaji Nyuki Afrika.
Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Toka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Prof. Sylvia Temu akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani)kuhusu mafanikio ya mradi wa Sayansi  Teknolojia na Elimu ya Juu ambao umeonyesha mafanikio kwa asilimia 90 ikiwemo ujenzi wa majengo ya Kisasa katika vyuo vya umma ikiwemo chuo Kikuu Huria, Chuo Kikuu Dar es Salaam na Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu Changombe,kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo, Bi Zamaradi  Kawawa. 
Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Toka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Prof.  Sylvia Temu akiwaeleza waandishi wa habari  leo Jijini Dar es salaam hawapo (pichani) kuhusu umuhimu wa jamii kuchangia katika sekta ya elimu ya Juu ili kupanua zaidi wigo wa wanafunzi wanaojiunga na Elimu  hiyo. (Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo)

Na Frank Mvungi-Maelezo
WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wahimiza wananchi kote nchini kushiriki katika ufugaji wa nyuki  ili kuongeza vipato vyao na kuchangia katika kukuza uchumi wa Taifa.
Hayo yamesemwa na Ofisa Ufugaji Nyuki Mwandamizi  wa wakala huo Bw. Steven  Msemo jana, jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kuhamasisha jamii kushiriki katika ufaugaji wa nyuki.
Akifafanua Msemo amebainisha kuwa mizinga ya nyuki takribani  14,000 imetengenezwa na kugawiwa wananchi wanaoishi jirani na Misitu ikiwa ni moja ya mikakati ya Serikali katika kukuza sekta hiyo.
“Wakala wa Huduma za misitu Tanzania kama Taasisi inayo mizinga 3,870 iliyo katika manzuki mbalimbali katika kanda saba na katika mashamba ya miti kwa lengo la kuzalisha na sehemu ya mafunzo kwa jamii “alisisitiza Msemo
Katika kuwajengea uwezo wananchi Msemo amebainisha kuwa Wataalamu wa ufugaji nyuki wamekuwa wakiwajengea uwezo wananchi kwa kuwapa mbinu za kusimamia makundi ya nyuki na kuzalisha malkia ili kuondokana na mazoea ya kutundika mizinga na kuacha hadi kipindi cha mavuno.
Aidha, Wakala  umekuwa ukihamasisha asasi zinazojikita na kutengeneza vifaa vya ufugaji nyuki kuzingatia utaalamu na vipimo vya mizinga.

Tanzania ni moja kati ya nchi zenye utajiri mkubwa wa makundi ya nyuki yenye uwezo wa kuzalisha asali na mazao mengine ya nyuki mfano Nta,Gundi ya nyuki na chavua.

No comments:

Post a Comment