TANGAZO


Thursday, October 9, 2014

Timu ya Viongozi wa Dini yajifua Morogoro kwa mpambano wao wa Oktoba 12, 2014 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kulia), akifanya mazoezi ya kuuzea mpira, wakati wa mazoezi ya timu hiyo, mjini Morogoro leo, kujiandaa na mchezo wa kirafiki kati ya viongozi hao, utakaofanyika Uwanja wa Taifa Jumapili Oktoba 12, kabla ya mpambano wa Timu ya Taifa na Benin. 
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, akituliza mpira kwenye kifua baada ya kurushiwa na mwalimu wa timu hiyo, Stefan Reith (kushoto), wakati wa mazoezi hayo.
Wachezaji Padri John Solomon (kushoto) na Sheikh Hassan Malangali wakiwania mpira wakati wa mazoezi hayo.
Shemasi Joas John (kulia), akiwania mpira na Mchungaji George Fupe, wakati wa mazoezi ya timu hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (kushoto), akizungumza na wachezaji wa timu ya Viongozi wa Dini, wakati wa mazoezi yao, mjini Morogoro leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Viongozi wa Dini, wakati wa mazoezi yao, mjini Morogoro leo. 

Nyendo Mohamed, Morogoro

MASHEIKH na Maaskofu wametua mjini Morogoro kuweka kambi kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya kirafiki baina yao, mchezo utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Oktoba 12, mwaka huu.

Mchezo huo, utachezwa ndani ya dakika sitini (60), huku kila mmoja ya wachezaji wa timu hizo, wakiahidi kuonesha mchezo mzuri wa kusisimua na wa kupendeza siku hiyo.

Akizungumza leo, mjini Morogoro kwenye mazoezi ya timu hiyo, Mkuu  wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadik, wakati alipotembelea mazoezi ya timu hizo, alisema kuwa timu itakayoshinda mpambano huo, itaibuka na kikombe huku timu nyingine ikipaata kifuta jasho.

Pia alisema kuwa jambo hilo ni kubwa sana kwani lengo la wananchi ni kupata ujumbe ambao ni Amani na Kushirikiana kwa pamoja bila kujali itikadi ya mtu.

''Jambo hili ni muhimu na kubwa mno na tunataka liwe endelevu, kwani litakuwa jambo jema litakalochangia amani hasa ukuzingatia mwakani utakuwa mwaka wa uchaguzi,''alisema Sadiki.

Alisema kuwa kwa kuwa jambo hilo, ndio linaanza mshindi atapata kikombe na aliyeshindwa atapata fedha kidogo, lakini utafanyika utaratibu mwakani kila mshiriki apate medali.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati, Sheikh Alhadi Mussa Salum alisema kuwa wamefika Morogoro salama na kuanza mazoezi na wanayafurahia mazoezi hao, hivyo watu watarajie mazuri siku ya mechi.

Sheikh Alhad, alisema kuwa tangu waanze mazoezi hayo, kuna mabadiliko kidogo, wamekuwa wapesi huku akisema yeye atacheza dakika zote sitini.

Hivyo kuwataka watu wajitokeze kwa wingi siku hiyo, kuangalia mchezo huo, kwani una lengo jema la kusambaza amani nchini bila kuangalia itikadi ya dini ya mtu yoyote.

Hata hivyo Mwalimu wa viongozi, Padri Richard Kamenya alisema kuwa amewanaoa vema wachezaji hao na ameona maendeleo tofauti na mwanzo, hivyo kusisitiza, kuwataka watu wasikose kujitokeza kwa wingi siku ya Jumapili kushuhudia mechi hiyo.

Timu za viongozi wa Dini zitakazomenyana siku hiyo ni za Amani Sports Club na Mshikamano Sports Club, huku viongozi wa dini zote wakichanganyika katika timu hizo, ikiwa ni ishara ya kuonesha suala zima la Amani na Mshikamano kati ya viongozi hao.

No comments:

Post a Comment