TANGAZO


Thursday, October 9, 2014

Ikulu, Hazina, Mahakama zatinga nusu fainali SHIMIWI

Kamati ya Waamuzi wa mchezo wa kuvuta kamba ikisubiri kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (hayupo pichani) aliyetembelea viwanja vya Jamhuri,Morogoro mapema jana kushuhudia michezo ya kuvuta kamba.
Mwamuzi wa mchezo wa kamba Bw. Ruvu Kiwanga (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil alipotembelea viwanja vya Jamhuri, Morogoro mapema jana.
Baadhi ya waamuzi wa mchezo wa kamba wakisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil alipotembelea viwanja vya Jamhuri, Morogoro mapema jana.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akikagua timu ya kamba ya Ikulu alipotembelea viwanja vya Jamhuri, Morogoro mapema jana.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akikagua timu ya kamba ya Wizara ya Kilimo alipotembelea viwanja vya Jamhuri, Morogoro mapema jana. 
Timu ya kamba ya Uchukuzi ikivutana na timu ya kamba ya Ujenzi (haipo pichani) katika mchezo wa SHIMIWI uliofanyika viwanja vya Jamhuri mjini Morogoro jana. Uchukuzi iliibuka mshindi kwa kuwa na pointi 1-0.
Timu ya kamba ya Ujenzi ikivutana na timu ya kamba ya Uchukuzi (haipo pichani) katika mchezo wa SHIMIWI uliofanyika viwanja vya Jamhuri mjini Morogoro jana. Uchukuzi iliibuka mshindi kwa kuwa na pointi 1-0.
Timu ya kamba ya Ujenzi ikifanyishwa mazoezi ya viungo baada ya kutoka droo katika mvuto wa kwanza na dhidi yake na timu ya kamba ya Uchukuzi.Uchukuzi ilishinda kwa pointi 1-0 baada ya kuivuta Ujenzi katika mvuto wa tatu.
Timu ya kamba ya Ujenzi ikifanyishwa mazoezi ya viungo baada ya kutoka droo katika mvuto wa kwanza na dhidi yake na timu ya kamba ya Uchukuzi.Uchukuzi ilishinda kwa pointi 1-0 baada ya kuivuta Ujenzi katika mvuto wa tatu.
Mashabiki wa mchezo wa kuvuta kamba wakiangalia timu zilizoshiriki kuvuta kamba kwenye uwanja wa Jamhuri,mjini Morogoro jana.
Timu ya kamba ya RAS Iringa ikivutana na timu ya kamba ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (haipo pichani) katika mchezo wa SHIMIWI uliofanyika uwanja wa Jamhuri,mjini Morogoro jana. RAS Iringa iliibuka mshindi kwa pointi 1-0.
Timu ya kamba ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ikivutana na timu ya RAS Iringa (haipo pichani) katika mchezo wa SHIMIWI uliofanyika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana. RAS Iringa iliibuka mshindi kwa pointi 1-0.

Na Happiness Shayo, Morogoro
TIMU za kamba za Ikulu, Hazina na Mahakama zimeingia hatua ya nusu fainali kwa kishindo baada ya kuzivuta timu pinzani katika michezo ya SHIMIWI iliyofanyika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana.
Michezo hiyo ya kusisimua iliyovuta mashabiki wengi ilianza majira ya saa moja asubuhi ambapo timu ya kamba ya wanawake ya Ikulu iliivuta timu ya kamba ya wanawake ya Kilimo na kuibuka mshindi kwa kuvuta mivuto yote miwili.
Mchezo wa pili ulikuwa kati ya timu ya kamba ya wanawake ya Wizara ya Ujenzi na timu ya kamba ya wanawake ya Wizara ya Uchukuzi zilizolazimishana kutoka droo kwa michezo miwili ya kwanza na hatimaye Uchukuzi kuibuka mshindi kwa mvuto mmoja baada ya kuvutana kwa mara ya tatu.
Katika mchezo mwingine timu ya kamba ya wanawake ya Wizara ya Mambo ya Ndani ililazimishana droo na timu ya wanawake ya RAS Iringa na kulazimu waamuzi kurudia mchezo huo na hatimaye RAS Iringa kuibuka mshindi kwa kuwa na pointi 1-0.

Mchezo mwingine ulichezwa kati ya timu ya kamba ya wanawake ya TAMISEMI ikiivuta timu ya wanawake ya Mahakama kwa mvuto mmoja.
Kwa upande wa timu za kamba za wanaume,Ikulu iliibuka mshindi baada ya kuivuta timu ya NFRA huku Uchukuzi ikiibuka mshindi baada ya kuivuta timu ya Afya kwa mivuto yote miwili.

Timu nyingine zilizoingia dimbani kwa upande wa timu za wanaume ni timu ya kamba ya Mahakama iliyoivuta timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani na kuibuka na pointi 2 huku timu ya kamba ya Hazina ikiivuta timu ya kamba ya Maliasili na kuibuka na pointi 2.

Timu za kamba kwa wanawake na wanaume jana zimetoana katika hatua ya robo fainali ambapo washindi wataingia nusu fainali itakayochezwa leo.

No comments:

Post a Comment