TANGAZO


Thursday, October 9, 2014

WIZARA YA FEDHA yatoa taarifa kuhusu kuanza Mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia na IMF jijini Washington DC nchini Marekani

                
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali  Dk. Servacius Likwelile akifurahia jambo na Bw. Herve’ Joly ambaye ni Mkurugenzi   msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki. Mara tu baada ya kuingia ukumbini. 

Dk. Servacius Likwelile, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa serikali  akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania. Kutoka kushoto ni Kamishna wa Bajeti Bw. John Cheyo akifuatiwa na Bi. Mwanaidi Mtanda ambaye ni mhasibu mkuu wa Serikali na wa mwisho kutoka kulia ni Balozi Liberata Mulamula. 
 Bw. Herve’ Joly ambaye ni Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki akishauriana na  mwenzake baada ya kupokea hoja kutoka kwa Dk. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali.

Balozi wa Tanzania nchini Marekani – Washington Mhe. Liberata Mulamula pamoja na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dk. Servacius Likwelile, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha wakifurahia pongezi walizopewa na ujumbe wa IMF kuhusu muelekeo mzuri wa uchumi wa Tanzania.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dk. Servacius Likwelile akielezea mikakati ya nchi ya Tanzania katika kuinua uchumi na kuongeza pato laTaifa kwenye Mkutano uliofanyika leo juu yuliohusu  masuala na fedha na sera ya kiwango cha ubalilishaji fedha.

Kila  mwaka Bodi ya Magavana ya Shirika la Fedha la Kimataifa na kundi la Benki ya Dunia hukutana kwa ajili ya kujadili  kazi za Taasisi zinazowahusu. Mikutano hii imeanza tarehe 06 Octoba na itafikia kilele chake hapo tarehe 13, mwezi Octoba, 2014.Mikutano hii hufanyika mjini Washington DC kwa miaka miwili mfululizo na kwa mwaka wa tatu hufanyika kwa nchi mwanachama. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile ndiye kiongozi wa ujumbe kutoka Tanzania na yeye anawakilisha kama Gavana mbadala (Alternate Governor) pamoja na Gavana wa Benki Kuu  Prof. Benno Ndulu  ambaye pia ni Gavana katika mikutano hii.
Mikutano hii inatoa nafasi ya kuweza kujadiliana na Benki ya Dunia pamoja na Shirika la Fedha la Kimataifa kuhusiana na hali ya uchumi kwa maana ya sera za fedha na sera za mapato na matumizi. Nia yao kubwa ni kutaka kusikia mawazo yetu kuhusu jinsi ya kuboresha uchumi ili wawe katika nafasi nzuri ya kuangalia ni wapi wanaweza kutusaidia kuboresha na kuona kwamba nchi yetu inaendelea kufanya vizuri zaidi. Maeneo ambayo yameshajadiliwa ni pamoja sera kuhusu kiasi cha ubadilishaji fedha, mapato ya nchi kwa ujumla na mwendo wa matumizi ya fedha.
Hali ya  utendaji wa kiuchumi na hali ya matumizi na mapato ya fedha ya Tanzania imeonekana ni ya kuridhisha  japo pado kunachangamoto ya ajira.
Hali ya hewa mjini  hapa ni baridi kiasi na manyunyu ya hapa na pale   
Imetolewa na:
Ingiahedi Mduma
Msemaji -Wizara ya Fedha
Washington D.C

7/10/2014

No comments:

Post a Comment