TANGAZO


Friday, October 3, 2014

TWPG yajivunia manufaa waliyopata wanawake katika Katiba inayopendekezwa

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Angellah Kairuki akitoa mada wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake  kuhusu maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Anna Abdalah akitoa mada wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake kuhusu maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014.
Mhadhiri Msaidizi wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Iringa, Bw. Dunford Mpelumbe akitoa mada wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge      Wanawake kuhusu maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akitoa neno la shukurani mara baada ya kumalizika kwa utoaji mada kuhusu maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Sophia Simba akichangia mada wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake kuhusu maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014.
Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Asha-Rose Migiro akichangia mada leo mjini Dodoma kuhusu maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Felister Bura akichangia mada wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake kuhusu maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014. 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Dkt. Angelina Samike akichangia mada wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake kuhusu maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014. 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Zainab Gama akichangia mada wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake kuhusu maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014. 
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakifuatilia mada na michango mbalimbali iliyokuwa ikiwasilishwa na baadhi ya wajumbe wa bunge hilo leo mjini Dodoma kuhusu maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014. 
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakifuatilia mada na michango mbalimbali iliyokuwa ikiwasilishwa na baadhi ya wajumbe wa bunge hilo leo mjini Dodoma kuhusu maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014. 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Fenella Mukangara (kulia) akisalimiana na mjumbe mwenzie wa Bunge hilo, Mhe. Angellah Kairuki mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake kuhusu maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014. 
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (kulia) akibadilishana mawazo na mjumbe mwenzie wa bunge hilo, Mhe. Martha Mlata mara baada ya kumalizika kwa mkutano kuhusu maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa wakati wa mkutano wa Umoja wa Wabunge Wanawake uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014. 
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakimshangilia Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta mara walipokutana nae nje mara baada ya kumaliza mkutano wao kuhusu maandiko ya kisera na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa uliofanyika mjini Dodoma leo 3 Septemba, 2014. (Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma)

Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.
03/09/2014.
UMOJA wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG) wamejipongeza kwa hatua kubwa waliyofikia na manufaa waliyoyapata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Wabunge hao ambao pia ni Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakati walipofanya semina iliyoandaliwa kwa ajili ya wajumbe hao kuhusu maandiko ya kisheria na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa.

Akitoa mada wakati wa Semina hiyo, Katibu Mkuu wa TWPG ambaye pia ni Mjumbe wa bunge hilo, Mhe. Angellah Kairuki amesema kuwa moja ya manufaa ambayo wanawake watayapata katika Katiba mpya ijayo ni kuhusu masuala ya uongozi ulio bora wenye kuzingatia sifa na weledi katika michakato ya ajira na uteuzi ambapo suala hilo limetiliwa nguvu katika Ibara ya 208, Ibara ndogo ya kwanza kipengele C ambapo katika masuala ya uteuzi na mambo ya ajira katika nafasi mbalimbali katika Utumishi wa Umma utazingatia uwezo wa kitaaluma, weledi, ujuzi, usawa wa jinsia hivyo suala la usawa wa jinsia limezingatiwa.

Mhe. Kairuki ameongeza kuwa, katika Sura ya Kumi inayohusu masuala ya Bunge kama ilivyoelezwa katika Ibara ya 129 ibara ndogo ya Nne, amesema kuwa kwa kutambua kuwa Bunge ndiyo mhimili muhimu wa dola, Katiba inayopendekezwa imekusudia kurekebisha kasoro iliyopo ya uwakilishi mdogo wa wanawake bungeni ambapo hivi sasa kuna asilimia 36.6% ya wanawake bungeni.
“Kupitia Katiba hii inayopendekezwa kupitia Ibara ya 129 Ibara ndogo ya Nne tutakuwa na uwakilishi uliosawa baina ya Wabunge wanawake na Wabunge wanaume”, alisema Mhe. Kairuki.

Aidha, alieleza kuwa katika Sura ya 12 inayohusu Mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tume ya Utumishi wa Mahakama imepewa wajibu katika ajira mbalimbali na uteuzi kuhakikisha kuwa inazingatia usawa wa jinsia.

Naye Mhadhiri Msaidizi wa Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Iringa, Bw. Dunford Mpelumbe amewapongeza wajumbe hao wanawake kwa kazi kubwa walioifanya katika kudai haki zao huku akizungumzia juu ya baadhi ya Mikataba ambayo Tanzania imeridhia pamoja na baadhi ya itifaki za Kimataifa yakiwemo maazimio mbalimbali ambayo Tanzania kama Mwanachama wa Jumuiya ya Kimataifa imeridhia na hatua kubwa iliyopiga.

Mpelumbe amesema kuwa katika Azimio la 1948 (Universal Declaration of Human Rights) katika Ibara yake ya kwanza inaelezea juu ya mambo ya usawa kati ya mwanamke na mwanaume, lakini pia suala la usawa kati ya binadamu wote umepewa kipaumbele.
Mpelumbe ameongeza kuwa licha ya Mikataba ya Kimataifa pamoja na sheria mama zilizopo sasa nchini, haki za wanawake zinatakiwa kujengewa ulingo wa kuzisemea mara kwa mara ili watu wapate kuzielewa vizuri.
“Nchi za wenzetu wameweka jitihada za dhati kabisa katika kujenga uwezo wa mwanamke na jitihada hizi zinatokana na utiaji sahihi na kuridhia hii Mikataba ya Kimataifa mbalimbali ambayo inatoa haki za wanawake lakini hatua ya pili ni kwa kuchukua hatua za msingi za kikatiba na kisheria kuziweka hizo haki za mwanamke katika ulingo wa Kimataifa zionekane zaidi na kwa uwazi kabisa katika Katiba ya nchi na Sheria za nchi”, alisema Mpelumbe.
Naye Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni mjumbe wa Bunge hilo, Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro amesema kuwa mshikamano ambao Wabunge wanawake wa Bunge hilo wameuonyesha ni mkubwa sana kwani wameweza kushikamana bila ya kujali Vyama walivyotoka, Kundi waliloliwakilisha , Sura na hata afya zao.

Dkt. Migiro ameeleza kuwa suala la hamsini kwa hamsini limekaa vema katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa na itawapa wanawake wengi msingi wa kuteremka chini kwani wanawake wengi wamejitokeza kwa wingi katika Mabaraza ya Kata na Taasisi zenye mrengo unaofanana na wamekuwa waaminifu ndani ya Bunge Maalum.
“Katiba hii ni yenu, tutakwenda kuipigia debe kwani ni Katiba ambayo imetuweka mahali pazuri kuimarisha haki ndani ya nchi yetu, maslahi ndani ya taifa letu, kuimarisha Muungano wetu na umoja wetu”, alisema Dkt. Migiro.

No comments:

Post a Comment