Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya KCB Tanzania, Godfrey Ndalahwa akiongea na wadau wa Taasisisi za kijamii (hawapo pichani)wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwaelimisha wadau hao jinsi ya kujiunga na Akaunti ya kijamii isiyokuwa na makato. Akaunti hiyo ni kwaajili ya Taasisi mbalimbali za Kijamii, zikiwemo mashule, NGO, Vikoba, Saccos. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya KCB Tanzania, Godfrey Ndalahwa akiwafafanulia Jambo
kwenye vipeperushi Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Heritage iliyopo
Banana Dar es Salaam,(katikati) Mkuu wa T-Marc Tanzania Ibrahim Toroka
vinavyoelezea jinsi ya kujiunga na Akaunti ya kijamii isiyokuwa na
makato akaunti hiyo ni kwaajili ya Taasisi mbalimbali za Kijamii
,zikiwemo mashule,NGO,Vikoba,Saccos. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa
wiki jijini Dar es Salaam.
Dar es Salaam, Juni 27, 2014
KATIKA kuboresho huduma za kijamii nchini
benki ya KCB Tanzania imewaletea wateja wake huduma mpya ya akaunti ya
jamii ambayo imelenga zaidi taasisi zenye malengo ya kuisaidia jamii
kama vile Elimu, Afya, kidini, manispaa, mashirika yasiyo ya kiserikali
(NGOs), SACCOS, VIKOBA, vilabu mbalimbali vya kijamii.
Hayo yalibahanishwa na
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Godfrey Ndalahwa wakati wa
hafla fupi ya chakula cha jioni iliyoandaliwa mwishoni mwa wiki kwa
ajili ya wateja wao jijini Dar es Salaam ambapo waliweza kufahamishwa
juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo ikiwemo akaunti mpya
za kijamii.
“Leo
tumekusanyika hapa katika hafla hii fupi ya chakula cha jioni kwa lengo
la kuongea na ninyi wateja wetu ili tubadilishana mawazo juu ya huduma
zetu za kibishara tunavyoendesha. Tumekuwa tukikutana na wateja wetu
mara kwa mara katika mikoa ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro,
Mwanza, Zanzibar na leo jijini Dar es Salaam.tukiwa na lengo kubwa la
kuwafikia wateja wengi zaidi kwa kuzungumza nao kwani tunaamini kwa
kufanya hivyo tutakuwa tumewasaidia zaidi jinsi ya kufanya biashaa na
kuweza kutunza fedha zao.” Alisema Ndalahwa
Akizungumzia
juu ya huduma mpya ya akaunti ya jamii, Mkurugenzi huyo alisema,
“Akaunti ya jamii (community account) ni sawa kabisa na ile ya biashara
(current account) lakini tofauti kubwa ni kwamba hii imeelekezwa zaidi
kuisaidia jamii. Hivyo basi, hii haina makato yoyote ya uendeshaji na
inatoa huduma zote shirikishi bure kabisa kama hundi, uhamishaji na
uingizaji wa pesa kutoka akaunti moja kwenda nyingine hapa nchini (TT).
Pia hakuna kiwango cha kufungulia akaunti, akaunti hii ni maalumu kwa
taasisi zenye kuleta mabadiliko katika jamii yaani taasisi zenye malengo
ya ustawi wa jamii kama vile; Taasisi za elimu, afya, kidini,
manispaa, mashirika yasiyo ya kiserikali, SACCOS, VIKOBA, vilabu mbali
mbali vya kijamii (social clubs) na kadhalika.
“Kuzinduliwa
kwa akaunti hii kunaambatana pia na mikakati ya benki ya KCB katika
kuisadia jamii yatu inayotuzunguka. Benki yetu kwa kulijua hili imeelekeza
misaada yake kwa jamii kupitia sekta muhimu zikiwemo elimu, afya,
mazingira , ujasiriamali na kusaidia maafa mbalimbali nchini. Kwa
kipindi cha miaka mitatu iliyopita
benki ya KCB imeweza kusaidia jamii kwa kutoa misaada mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya Sh. Bilioni 1.0 ” Aliongezea
Kwa
upande wa kuisaidia jamii Bw. Ndalahwa alielezea kuwa wanafahamu kwamba
si rahisi kuondoa kabisa matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii yetu
kwa mara moja. Kikubwa wanachokiamini ni kuwa jitihada za kufanya hivyo
zinatakiwa ziwe endelevu hadi pale matatizo hayo yatakapotokomea kabisa
na benki yake itakuwa mstari wa mbele katika hilo.
“Mkurugenzi huyo alitoa wito kwa
shule mbalimbali, hospitali na vituo vya afya mbalimbali, taasisi za
kidini, mashirika yasiyo ya kiserikali, Vikoba, SACCOS kujaribu kutumia
akaunti halafu mjionee kama mtatamani tena akaunti ya biashara ya
kawaida. Pia tuna akaunti nyingine nzuri sana kama akaunti yetu ya akiba
inayoitwa simba servers – ambapo unapata asilimia 6-7.” Alisema.
Mbali
na kuwa na matawi mbalimbali nchini, huduma za benki ya KCB pia
zinapatikana katika nchi sita za Afrika yaani; Kenya, Uganda, Rwanda,
Burundi na Sudani Kusini ambapo huduma zake ziko kidigitali zaidi.
No comments:
Post a Comment