Mshindi wa taji la Redds Miss Kanda ya Nyanda za Juu Kusini mwaka
2014, Maureen Godfrey akiwapungia mkono wadau wa urembo katika ukumbi
wa Highlands usiku wa kuamkia jana baada ya kutangazwa mshindi (Picha
zote na Francis Godwin)
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Gerald Guninita (kulia), akimpongeza mshindi wa taji la Redds Miss kanda ya
nyanda za juu kusini mwaka 2014 Maureen Godfrey baada ya kutawazwa
mshindi usiku wa
kuamkia jana.
Na Francis Godwin, Iringa
ZOEZI
la kumsaka Redds Miss kanda ya nyanda za juu kusini limekamilika kwa
Redds Miss Njombe 2014 Mrembo Mauren Godfrey kutoka mkoa wa Njombe
kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika kinyang'anyiro hicho .
Huku
mkoa wa Iringa ukiwakilishwa na Martha John aliyekuwa Redds Miss
Iringa 2014 na mkoa wa Ruvuma ukiwakilishwa na mrembo wake Naba
Magambo ambae ni Redds Miss Ruvuma 2014 kwa ushindi huo warembo hao
wa tatu ndio watakaopeperusha bendera ya urembo ya mikoa ya nyanda
za juu kusini katika kinyang'anyiro cha kumsaka Redds Miss
Tanzania 2014
Katika
shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia jana katika ukumbi wa
Highlands mjini Iringa na kushuhudiwa na kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa
Gelard Guninita mrembo Maureen aliweza kumpokea taji hilo aliyekuwa
Redds Miss Kanda ya nyanda za juu kusini mwaka 2013 Lina Allan ambae
alipokea taji hilo mwaka 2011 kutoka kwa Christine Wiliam .
Katika kinyang'anyiro hicho warembo Salome George ,Magreth Tarimo,Naba
Magambo,Elizabeth Mussa,Maureen Godfrey,Martha John,Juliana
Gilbert,Flaviana Msalila,Faina Salum na Atukuzwe Fabian ndio
ambao walifanikiwa kuingia hatua ya kumi bora na kupelekea kuingia
katika wakati mgumu zaidi wa kuenguliwa kwa maswali.
Katika hatua hiyo ya kumi bora majaji walilazimika kufanya mchujo na kuwapata watano bora ambao ni Maureen Godfrey,Naba Magambo,Faina Salum,Atukuzwe Fabian na Martha John kabla ya kumpata mshindi wa kwanza hadi tatu kwa njia ya maswali .
Maureen
na wenzake wawili waweza kung'ara zaidi katika kinyang'anyiro
hicho baada ya kuonyesha uwezo mkubwa wa kujibu maswali na kujieleza
zaidi na kupewa baraka za kuiwakilisha kanda ya nyanda za juu kusini
katika kinyang'anyiro
kama hicho ngazi ya taifa .
Awali mratibu wa mashindano hayo
Doss Magambo alisema kuwa mshindi wa kwanza katika kinyang'anyiro
hicho atazawadiwa kiasi cha Tsh milioni 1 wakati mshindi wa pili
atazawadiwa kiasi cha Tsh 500,000 na mshindi wa tatu atazawadiwa kiasi
cha Tsh 300,000 huku kila mshiriki atapewa kiasi cha Tsh 80,000 kama
kifuta jasho zoezi ambalo litafanyika siku moja baada ya shindano.
No comments:
Post a Comment