TANGAZO


Sunday, April 20, 2014

Watu kadhaa wauawa nchini Sudan kusini

 

Tatizo la wizi wa mifugo ni kubwa katika jimbo la Warrap
Idadu kubwa ya watu wameuawa wakati wa jaribio la wizi wa Ng'ombe katika jimbo la Warrap nchini Sudan Kusini.
Afisa mmoja katika eneo hilo Paul Dhel Gum ameviambia vyombo vya habari kwamba takriban watu 28 wameuawa.
Amesema kuwa polisi wamewaua wavamizi wengi.
Uvamizi huo ulitekelezwa katika eneo la mashambani la jimbo la Warrap siku ya alhamisi ,na kwamba hakuna maelelzo zaidi.
Haijulikani iwapo mauaji hayo yanashirikishwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya serikali ya Sudan kusini na waasi walio watiifu kwa aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar.

No comments:

Post a Comment