Baadhi ya waombolezaji wakibadilishana mawazo. Katikati ni mwanamuziki wa Skylight band, Joniko Flower.
Waombolezaji wakiendelea kubadilishana mawazo wakati wakisubiri mwili wa marehemu kufika. Mwenye baibui nyeusi ni mke wa Chicago Matelephone na wanamuziki wa Skylight band.
Mkurugenzi wa Skylight Band, akijadili jambo na Aneth Kushaba ili kuweka mambo sawa kabla ya mwili wa marehemu kuwasili.
Mchungaji wa Kanisa alipokuwa anasali marehemu Challa, akiongoza ibada ya kumuombea marehemu Ayoub Songoro maaruf Chill Challa aliyekuwa mwanamuziki na mpiga gita wa Skylight Band.
Jenenza la Challa likiingizwa kaburini. |
MPIGA gitaa wa bendi ya Skylight, aliyefariki juzi katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, Chiri Challa, amezikwa katika makaburi ya Mwananyamala kwa Kopa, Kinondoni jana na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.
Awali uongozi wa bendi hiyo kupitia kwa Meneja wake, Aneth Kushaba ‘AK47’, ulieleza kuwa mwanamuziki huyo alifariki kutokana na ugonjwa wa kupooza nusu ya mwili wake, hali iliyosababisha kutofanya kazi ipasavyo.
Kushaba alibainisha kuwa kupooza huko kulisababisha mishipa ya damu kichwani kupasuka na kumsababishia maumivu makali sehemu za kichwani.
“Tunatoa pole kwa familia ya marehemu na mashabiki wetu wote katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa mpendwa wetu,” alisema Kushaba.
No comments:
Post a Comment