TANGAZO


Sunday, April 20, 2014

Shamba la mkulima lavamiwa na kufyekwa mazao Chamwino, Dodoma

Mmiliki wa shamba la chakula na Biashara Msafiri Khatib akionesha uhalibifu uliofanywa na wavamizi waliovamia na kufyeka mazao yote katika shamba lake lote lenye ukubwa wa Hekar 13 na kisha kutokomea. (Picha zote na John Banda, Dodoma)

Mke wa mwenye Shamba lililovamiwa na kufyekwa mazao yote, Meresiana Kalunju akiwa ameshika moja ya nguzo zilizokuwa zimeshika Kibanda walichokuwa wakikitumia kuishi shambani hapo kikiwa kimechomwa na moto wa Petrol. 
Wanafamilia wakijadili jambo katika shamba la Msafiri Khatibu, lililofyekwa mazao yote na watu waliovamia saa 9 mchana wakiwa na silaha na kisha kutokomea kwenye magari waliyokuwa nayo.
Msafiri Khatib akionyesha Mahindi yaliyokwisha haribika kwa kuingia maji siku tatu baada ya kufyekwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni mgambo, wanajeshi wa Jeshi la wananchi (JWTZ) na Polisi waliovamia saa 9 mchana huku miongoni mwao wakiwa na Bunduki tatu huku wakiyaacha mashamba mengine yaliyoozunguka shamba hilo.
Mmiliki wa shamba la chakula na Biashara Msafiri Khatib akionyesha uharibifu uliofanywa na wavamizi waliovamia na kufyeka mazao yote katika shamba lake lote lenye ukubwa wa ekari 13 na kisha kutokomea.
Shemeji wa Msafiri Khatib,  Jema Kalunjuu akiwa shambani hapo kwa masikitiko, wakati akiangalia jinsi uharibifu wa mazao ulivyofanywa wiki iliyopita.

Na John Banda, Chamwino
WATU wanaodhaniwa kuwa ni migambo, polisi na wanajeshi wa Jeshi la wananchi (JWTZ) wakiwa na Bunduki walivamia shamba la Mkulima Msafili Khatib lenye ukubwa wa hekar 13 na Kufyeka mazao yote yaliyokuwa shambani humo yakiwemo Mahindi yaliyokuwa yamekomaa na kuchoma vibanda 2 kwa moto wa Petrol na kuiacha familia hiyo ikikosa makazi na chakula.


Tukio hilo lililotokea katika kijiji cha Chenene Walayani Chamwino
Dodoma Wiki iliyopita linahusishwa na viongozi wa kijiji hicho akiwemo Afsa Mtendaji Ester Mhwaji na Mwenyekiti wa Kijiji Gilbert Chitung’ati.


Akiongea kwa Masikitiko kuhusiana na Tukio hilo Khatib alisema April 14, 2014 saa 9 alasili Dk chache baada ya kutoka kuzozana na Afsa mtendaji aliyekuwa akimlazimisha Mmoja wa Maofisa Toka Wakala waBarabara aliyefika kumsainisha ili baada ya mavuno alipwe fidia ya shamba lake.


Alisema yeye akiwa hapo shambani alishtukia kundi kubwa la watu
wanaokadiliwa zaidi ya 30 wakiwa na mapanga na mafyekeo huku watatu kati yao wakiwa na Bunduki mkononi walifika na kuanza kufyeka mazao yake huku wakimkejeli nay eye awasaidie kazi hiyo walipomaliza azma yao na kuhakikisha wamechoma kwa moto wa petrol vibanda 2 walivyokuwa kitumia kwa makazi wakaondoka.


‘’Walifika watu hao na watatu kati yao walikuwa na Bunduki mkononi, waliokua wamevalia sale za polisi, za jeshi la wananchi (JWTZ) na za mgambo huku wengine walivaa za kawaida kitendo hicho kimenitia umasikini na kunifanya niishi kama wanyama na familia yangu yenye watoto 5 kwa kukosa pa kulala na chakula kwani tayali mahindi yalishakomaa na tulikuwa tunayala’’, alisema


Naye Meresiana Kalunju Mke wa mkulima huyo alisema tukio hilo
lilitokana na chuki za viongozi wa Serikali ya kijiji hicho cha
Chenene Afsa mtendaji na Mwenyekiti ambao kwa makusudi waliamua kumlazimisha Mumewe akubali fedha za fidia ya shamba hilo zipitie mikononi mwao ndipo azipate na alipokataa wakaamua kumkomoa kwa njia hiyo.
 

Alisema mtendaji aliwaambia eneo hilo lipo sehemu ya hifadhi hivyo watu wa maliasili watafika mashambani  na watakachokifanya wawaache, lakini cha kushangaza wamefyeka mazao yao tu huku wakiacha mashambammengine  yaliyozunguka shamba lao likiwemo la Mjumbe wa kamati ya Misitu John Selemani  kisa wachina wamechagu eneo hilo ili kujenga kiwanda cha Kokoto.

‘’Mwandishi tusingeweza kukubali fedha hizo zipitie mikononi mwa
viongozi hao kwa sababu mwezi wa pili mwaka huu Kampuni ya kichina iliwaliwapa viongozi hao malipo ya eneo la mashamba ya wananchi ili waweke makambi yao kwa ajili ya ujenzi wa barabara, chakushangaza mtendaji akali watu 70,000 kwa heka moja na wengine kulipwa 200,000 heka 5 tukalalamika ndiyo sababu Tanroad wamekuja kusimamia ulipaji huu’’,alisema.


Aidha alisema shamba hilo la hekari 13 lifanyiwa udhamini  siku hiyo, waliambiwa kati ya mwezi wa 6,7 watakapovuna ujenzi wa kalai la kusagia kokoto utafanyika mara baada ya kulipwa na ofisi ya Wakala wa Barabara kwa mkataba wa miaka 3 baada ya hapo watarudishiwa maeneo yao.


Akizungumzia tukio hilo Afsa Mtendaji wa kijiji hicho Ester Mhwaji
alisema ameshtushwa na tukio hilo na Vilevile anasikitishwa na meseji ambazo alipokea zikimuonya kutokubali Mkulima huyo kulipwa fidia ya mazao na Aridhi jambo ambalo aliamua kuliwekla wazi kwa wathamini waliotoke manispaa.


‘’Tulipomaliza na Yule Mthamini tuondoka na baadae nikajulishwa juu ya tukio hilo, na vitisho vikafuata toka kwa wakulima  nikiambiwa nitachomwa mishale na usiku nisitoke kujisaidi la sivyo nitauawa hali iliyonifanya kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi’’


‘’,Lakini Nimeshangazwa sana na kwa ajili ya usalama wangu naomba nisiwataje lakini hapa nina ujumbe wa maandishi kwenye simu ulionionya nisikubali mkulima Msafili Khatib Alipwe fidia, lakini pia sina cha kufanya maana jioni ya siku hiyo nilipokea ujumbe wa simu toka namba nisiyoijua ukinijulisha kuwa misitu wamefyeka mazao Chenene na Solow, na kwanini wafyeke mazao yaliyopo shamba moja tu?’’, alihoji Ester.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Gilbert Chitung’ati alisema hawezi
kuzungumzia swala hilo hata kama halikupitia ofisi ya mtendaji kwa
sababu lilitokea ngazi za juu.


Mkurugenzi wa Wilaya ya Chamwino alisema huyo mkulima ni haki yake kulipwa fidia na kwa kuwa ndiyo kwanza amelipata atalifuatilia ili ajue nani na kwanini wamefyeka ndipo atachukua hatua juu ya tukio hilo.


Kampuni ya Kichina ya Chico iliyoweka kambi katika kijiji hicho cha Chenene ndiyo iliyopewa tenda ya kuchonga Barabara ya kiwango cha Lami kati ya kijiji mtungutu na babati.

No comments:

Post a Comment