TANGAZO


Sunday, April 20, 2014

Wanahabari wasimulia masaibu yao Syria

 


Wanahabari walioachiliwa na watekaji nyara nchini Syria wawasili Ufaransa

Wanahabari wanne wa Ufaransa walioachiliwa baada ya kutekwa nyara na wanamgambo nchini Syria karibia mwaka mmoja uliopita wamewasili nchini Ufaransa.
Waandishi hao wamekuwa wakisimulia masaibu yao walipokuwa mikononi mwa watekaji wao wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kiisilamu wenye uhusiano na kundi la Al Qaeeda.

 
Mmoja wa waandishi hao, Didier Francois, alisema kuwa walifungwa kwa minyororo kwa pamoja na kufungiwa katika chumba kisicho na mwangaza
Mwenzake Nicolas Henin, alisema kuwa watekaji wao hawakuwatendea vizuri.
Bwana Henin na Francois wakiandamana na Edouard Elias na Pierre Torres, waliamkuliwa na familia zao pamoja na Rais Francois Hollande walipowasili nchini Ufaransa.

Kuokolewa

Walipatwa na wanajeshi wa Uturuki wakiwa katika mpaka wa Syria na Uturuki
Kundi la wapiganaji la 'Islamic State of Iraq' lenye uhusiano na kundi la Al Qaeeda limetuhumiwa kwa utekaji huo.
Picha za wanaume hao ziliwaonyesha wakiwa wamechakaa ingawa walikuwa bukheri wa afya.
Bwana Francois,mwenye umri wa miaka 53, alisema alikuwa na furaha sana kwani yuko huru, ameweza kuona mbingu, kutembea na kuzungumza bila kikwazo chochote.
"tuliishi kwa miezi sita gizani huku miezi miwili na nusu tukiwa tumefungwa kwa minyororo,'' aliambia kituo kimoja cha redio anachokimiliki.
"tuliona siku ndefu , ingawa hawakuwahi kupoteza matumaini,'' aliongeza bwana Francois.
Waandishi hao walipatikana wakiwa wamefunikwa nyuso zao na kufungwa minyororo katika sehemu moja ya mpakani mwa Syria na Uturuki.
Waliokolewa na wanajeshi wa Uturuki.
Wanaume hao walitoweka katika matukio mawili tofauti mwezi Juni mwaka jana.
Bwana Francois, ni mwandishi mwenye uzoefu wa miaka mingi na Elias ni mpiga picha. Wote walitekwa nyara wakielekea mjini Aleppo.
Henin, alikuwa anafanya kazi na jarida la Le Point huku bwana Torres, akiripotia kituo cha televisheni cha channel Arte, walitekwa nyara baadaye mwezi huo karibu na eneo la Raqqa.
Zaidi ya waandishi 60 wameuawa nchini Syria tangia kuanza kwa mgogoro dhidi ya serikali ya rais Bashar al Asaad miaka mitatu iliopita

No comments:

Post a Comment