Ofisa Uhusiano Manispaa ya Ilala Bi. Tabu Shaibu akiwaeleza
waandishi wa Habari (hawapo pichani)kuhusu mpango wa serikali wa kuendelea
kuimarisha Masoko katika Jiji la Dar es Salaam, Wakati wa Mkutano uliofanyika
katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Afisa Masoko wa Manispaa hiyo Bw. Athuman Mbelwa.
Na Frank Mvungi- Maelezo
SERIKALI yaimarisha masoko 18 katika jiji la Dar es salaam
katika kukabiliana na Ongezeko la Mahitaji ya Wananchi.
Hayo yamesemwa na Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala Bi
Tabu Shaibu wakati wa mkutano nawaandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Akifafanua Bi Shaibu amesema masoko makubwa ni 5 ambayo ni Buguruni,Ilala,Ferry,Kisutu na
Mchikichini ambapo jumla ya wafanyabiashara
wanaotumia masoko hayo ni 8,432.
Akieleza zaidi Bi
Shaibu alimesema kutokana na Utafiti uliofanywa na Ofisi ya Biashara ya
Manispaa ya Ilala mwaka 2009,ilibainika kuwa jumla ya wafanyabishara 21,500
hawana maeneo ya kufanyia biashara na wanatumia hifadhi ya barabara na maeneo
yasiyoruhusiwa kufanya biashara.
Kutokana na hali hiyo Bi Shaibu alibainisha kuwa katika
bajeti ya 2013/2014 jumla ya sh.Milioni
240 zilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa mabanda ya masoko ya Pugu ,Kigogo
fresh,Kiwalani na Kinyerezi ambapo wakandarasi wameshaonyeshwa maeneo ya
ujenzi kwa njia ya zabuni.
Katika hatua nyingine Bi shaibu alisema sh. Milioni 170
zimetumika kuboresha soko la Samaki feri kwa ajili ya ujenzi wa zoni ya kukaangia samaki baada ya kuungua.
Pia sh. Milioni 75 zilitumika. kuboresha mifereji ya maji
taka,ukarabati wa meza 23 za kunadia samaki,kuzibua mitaro ya maji taka na maji
ya mvua.
Ni jukumu la wafanyabiashara wote kuzingatia usafi kwa
kuhakikisha kuwa taka zinazozalishwa katika masoko yote zinahifadhiwa katika
maeneo husika na kutunza mazingira ya maeneo ya masoko ili kuwalinda watumiaji
wa huduma zinazotolewa katika maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment