TANGAZO


Tuesday, April 22, 2014

Mkutano wa Shirika la Reli Tanzania katika mkamkati wa mpango wa kukarabati na kuboresha Reli

Meneja mahusiano wa Shirika la Reli  Tanzania Midladjy Maez akiongea na washiriki wa semina ya mpango wa kukarabati reli ya kati itakayowasaidia wajisiria mali wa Tanzania, Kongo, Burundi na Rwanda leo jijini Dar es Salaam, mpango huo ni muendelezo wa jitihada ya kuboresha miundo mbinu ya reli ya kati.
Baadhi ya waandishi wa habari na washiriki wa mkutano wa Shirika la Reli Tanzania wakisikiliza kwa makini  hotuba ya mgeni rasmi  (hayupo pichani), wakati wa semina ya mpango wa kukarabati na kuboresha reli ya kati ili kuimarisha uchumi wa nchi leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, ambaye alikuwa mgeni rasmi Shaabani Mwinjaka, akiongea na washiriki wa semina ya mpango wa kuimarisha usafiri wa reli ya kati kwa ajili ya kusaidia usafiri kwa wajasiria mali,leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa semina ya mpango wa kuimarisha usafiri wa reli ya kati kwa ajili ya kusaidia usafiri kwa wajasiria mali wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi (hayumo pichani), leo jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, ambaye alikuwa mgeni rasmi Shaabani Mwinjaka, (mstari wa mbele wa nne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina ya mpango wa kuimarisha usafiri wa reli ya kati,leo jijini Dar es salaam. (Picha zote na lorietha Laurence-maelezo)

No comments:

Post a Comment