Mwenyekiti wa Baraza la Maichezo Zanzibar BMZ Bi Sherry Khamis,
akizindua Bonaza la Ziro Tatu kwa Vijana Kupiga Vita Maambukizo ya
Ukimwi Zanzibar,akirusha mpira kulizindua kwa mpira wa peti, Bonaza hilo
limeandaliwa na Jumuiya ya ZAYADESA, katika viwanja vya amani nje.
Mratibu wa miradi wa ZAYEDESA nDG. Mgoli Lucian akielezea madhumuni ya
Bonaza hilo la Ziro Tatu , na kutoa maana ya ZIRO TATU, ziro ya kwanza
ni Kuondoa Unyanyapaa, Ziro ya Pili Kupunguza Vifo kwa Maambukizo ya
Ukimwi na Ziro ya Tatu kupunguza na kuondoa Maambukizo kutoka kwa Mama
kwenda kwa Mtoto Zanzibar. Bonaza hilo limefanyika viwanja vya nje
uwanja wa Amani Zanzibar. (Picha zote kwa hisani ya ZanziNews Blog)
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Bi. Sherry Khamis, akitowa
nasaha zake kwa Vijana wanamichezo walioshirika Bonaza hilo, na
kushirikisha michezombalimbali ya Vijana kuhamasisha kuondoa maanbukizo
ya Ukimwi kwa Vijana wa Zanzibar.
Katibu wa Jumuiya ya ZAYEDESA Bi. Lucis Majaliwa akizungumza wakati wa
uzinduzi wa Bonaza hilo lililozinduliwa na Mwenyekiti wa Baraza la
Michezo Zanzibar, katika viwanja vya nje Amani Zanzibar, jumla ya Vijana
400, wameshiriki katika Bonaza hilo.
Washiriki wa Bonaza hilo wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar akitowa nasaha zake.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Bi. Shery Khamis akiwasalimia
baadhi ya Wanamichezi walioshiriki Bonaza hilo baada ya kulizinduwa
katika viwanja vya Amani Zanzibar.
Mratibu wa Miradi wa ZAYEDESA Ndg. Mgoli Lucian, akiongozana Wafanyakazi
wa ZAYEDESA, kuwasalimia wanamichezo walioshiriki Bonaza hilo la Ziro
Tatu.katika viwanja vya Amani.
Washiriki wa Bonaza la Ziro Tatu, wakishiriki mchezo wa netiboli kati ya
timu ya Amani na Mpendae, Mchezaji wa timu ya Mpendae akiwa na mpira
huku mchezaji wa timu ya Amani, timu Mpendae imeshinda 15-9
No comments:
Post a Comment