Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mary Daffa (kushoto) na Dk. Jasmine Tiisekwa, wakizungumza jambo wakati wakielekea kwenye ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kikao cha kuchangia Sura ya Kwanza na ya Sita za Rasimu ya Pili ya Katiba, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mohamed Seif Khatib (kushoto) na Steven Wassira, wakifuatilia michango ya wajumbe wenzao, iliyokuwa ikitolewa kwenye kikao cha bunge hilo leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakifuatilia michango ya wajumbe wenzao, iliyokuwa ikitolewa kwenye kikao cha bunge hilo, ukumbini humo leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakiwa kwenye ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kikao cha kuchangia vifungu vya Sura ya Kwanza na ya Sita vya Rasimu ya Pili ya Katiba, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakifuatilia michango ya wajumbe wenzao, waliyokuwa wakiitoa katika kikao cha bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri wa Sheria na Katiba, Asha Rose Migiro, akimweleza jambo mjumbe mwenzake, Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba, wakati wa kikao hicho.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Rashid Mtuta, akichangia vifungu vya Sura ya Kwanza na ya Sita vya Rasimu ya Pili ya Katiba, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mohamed Seif Khatib, akichangia vifungu vya Sura ya Kwanza na ya Sita vya Rasimu ya Pili ya Katiba, wakati wa kikao hicho.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Hamis Dambaya, akichangia vifungu vya Sura ya Kwanza na ya Sita vya Rasimu ya Pili ya Katiba, katika kikao cha bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, kutoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Mwalimu Ezekiah Oluoch, akizungumza na waandishi wa habari, mjini Dodoma leo, kuhusu suala la kuwataka viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kurudi bungeni kuendelea na mchakato wa Katiba kwa ajili ya kudumisha umoja na mshikamano wa nchi pia amewaonya wajumbe wanaotumia lugha za matusi katika michango yao bungeni humo kuacha suala hilo.












No comments:
Post a Comment