TANGAZO


Friday, April 25, 2014

SATF yatumia zaidi ya 11 mil kuwawezesha watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi

Na John Banda, Dodoma
ZAIDI ya million 11,7 zimetolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la
Social Action Trust Fund (SATF), linalo jishughulisha na kufadhili
watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi kwa asasi ya Kanisa la
Free Pentecosti Tanzania kwa ajili ya kutekeleza mradi mbalimbali ya elimu.
Akizungumza na wazazi, walezi na wanafunzi katika hafla ya ugawaji wa vifaa vya elimu kwa watoto wanaishi katika mazingira
hatarishi, Mkurugenzi wa Asasi ya kanisa hilo la FPCT Chamwino mjini Dodoma.
Stanley Mwailah alisema kiasi hicho cha fedha kilitolewa ili
kutekeleza mradi wa elimu kwa kipindi cha miezi sita kuanzia January 2014 hadi juni 2014 kwa ajili ya kulipia ada na vifaa vya shule za watoto 7 ya msingi  na watoto 49 wa sekondari za Manispaa ya Dodoma na Wilaya ya Chamwino.


Mwailah alisema kuwa mradi huyo wa Satf  kwa kushirikiana na Asasi ya FPCT,imefanikiwa kuwafikia walengwa wote kama ilivyopangwa kwenye mpango kazi kwa ajili ya kuwapatia misaada mbalimbali ya kielimu.
Alisema misaada iliyotolewa kwa ajili ya kila mtoto kwa mwanafunzi wa shule ya msingi kwa kipindi cha mwezi january hadi juni ni pamoja na, sare ya shule,daftari kubwa,peni,peseli vifutio mikebe na sweta.
Kwa upande wa shule za sekondari za kutwa kidato cha kwanza hadi cha nne, daftari za kauta,sare za shule,viatu, bengi,sweta na rula,pamoja na kuwalipia ada na michango ya mitihani ya Taifa na mock.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo wa asasi alisema pamoja na ufadhiri huo bado kuna changamoto kwa wanafunzi wa kike wa shule za sekondari kupata mimba na kusababisha walio wengi kuacha masomo.
Aidha alisema pia ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne bado ni
changamoto mfano mwaka 2013 waliomaliza walikuwa 34 waliopata daraja la pili ni 2 daraja la tatu ni 5 na nne ni 7 waliofeli na kupata alama ya sefuli ni 20.

No comments:

Post a Comment