TANGAZO


Saturday, April 5, 2014

Kuagwa na mazishi ya Askofu Godfrey Mdimi Mhogolo wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dodoma

Jeneza likiwa na  mwili wa aliyekuwa Askofu wa Kanisa la Anglican Dayosisi ya Dodoma Godfrey Mdimi Mhogolo aliyefariki wiki iliyopita nchini Afrika Kusini alikopelekwa kwa matibabu likiwa ndani ya kanisa kuu la Roho Mtakatifu wakati wa ibada maalumu. (Picha zote na John Banda, Dodoma)
Waumini na viongozi wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Kati wakilishusha Jeneza lilibeba mwili wa aliyekuwa askofu wa kanisa hilo Godfrey Mhogolo ulipofikishwa kwa mara ya kwanza tokea alipofariki nchini Afrika Kusini kanisani hapo kwa ajili ya kufanyiwa ibada ya maombezi.
Waumini wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi Kati, wakiwa kwenye mahema yaliyowekwa nje ya kanisa kuu la Roho Mtakatifu walipokuwa wakifuatilia ibada ya kuuombea mwili wa aliyekuwa Askofu wa Kanisa hilo Kanda ya Dodoma aliyefariki wiki iliyopita alipokuwa kwenye matibabu nchini Afrika ya Kusini.
Wageni mbali mbali kutoka nje ya nchi wakiwa ndani ya Kanisa la Roho Mtakatifu kwa ajili ya ibada maalumu ya kuuombea mwili liyekuwa Askofu wa Kanisa hilo, Godfrey Mhogolo aliyefariki wiki iliyopita alipokuwa kwenye matibabu Afrika Kusini.
Waumini wa kanisa hilo wakiwa ndani ya hema lilijengwa katika eneo la makaburi ya kuzikia viongozi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Kati ambapo walikuwa wakiandaa sehemu ya kuuzikia mwili wa aliyekuwa Askofu wa Kanisa hilo Godfrey Mhogolo unaotarjiwa kuzikwa leo Jumamosi.
Wachungaji na Makasisi wa Kaanisa la Anglikana Dayosisi ya Kati wakiwa wamejipanga nje ya kanisa la Roho mtakatifu mjini Dodoma kwa ajili ya kuupokea mwili aliyekuwa Askofu wa Kanisa hilo Godfrey Mhogolo. 
Ndani ya kanisa la Roho mtakatifu, waumini wakifuatila ibada ya kuuombea mwili wa aliyekuwa askofu wa kanisa hilo, Godfrey Mhogolo aliyefariki wiki iliyopita akiwa kwenye matibabu nchini Afrika Kusini. 
Wageni mbalimbali kutoka nje ya nchi, wakiwa ndani ya kanisa la Roho Mtakatifu kwa ajili ya ibada maalumu ya kuuombea mwili liyekuwa Askofu wa Kanisa hilo, Godfrey Mhogolo aliyefariki wiki iliyopita alipokuwa kwenye matibabu Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment