* Profesa Shivji nje
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania, (MCT), Kajubi Mukajanga, akizungumza na waandishi wa habari, mjini Dodoma jana, kuhusu uteuzi wa wajumbe wa Jopo la Wajuzi la MCT pamoja na mtazamo wake kuhusu hali ya majadiliano ya vifungu vya Sura ya Kwanza na ya Sita vya Rasimu ya Pili ya Katiba kwenye kamati yake namba nne pamoja na mambo mbalimbali ya yanayotokea kwenye kamati nyingine za bunge hilo.
Na Magreth Kinabo –Dodoma
Baraza la Habari Tanzania (MCT), limetangaza majina saba ya wajumbe wapya ya Jopo la Wajuzi wa uhuru wa habari wa kujiendeleza.
Majina hayo yametangazwa leo na Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Bunge mjini Dodoma.
Aliyataja majina hayo kuwa ni Profesa Penina Mlama, Jenerali wa Ulimwengu, Profesa Ruth Meena, Alli Ahmed Uki, Bonaventura Rutimwa, Ndimara Tigambwage na Wangethi Mwangi.
“jopo hili limechaguliwa kutokana na vigezo vya vya kuleta tija, ujuzi na kuibua masuala mapya ya kuipeleka mbele tasnia habari,”alisema huku akiongeza kwamba huteuliwa kila baada ya miaka mitatu.
Mukajanga aliwataja wajumbe wa awali kuwa ni Profesa Issa Shivji, Profesa Robert White, Profesa Palamagamba Kabudi, Penina Mlama, Saida Yahya, Wangethi Mwangi, Jenerali wa Ulimwengu na Dk.Peter Mwesige.
Wakati huohuo akizungumzuia kuhusu mchakato wa Katiba mpya kwa maoni yake aliwataka Watanzania kuondoa hofu kutokana na kelele zinatokea katika Bunge Maalum la Katiba kwa kuwa ndiko kutakakosaidia kupatikana kwa Katiba bora ya wananchi kwa msingi wa kuridhiana badala inayotokana na kikundi fulani.
Aliwataka baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo ,kuacha kuleta masuala ya kisiasa katika Bunge hilo, kwa sababu ni la maridhiano.
No comments:
Post a Comment