TANGAZO


Monday, April 21, 2014

Kongamano la Kitaifa linalozungumzia Rasimu ya Pili ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lafanyika Zanzibar

Mwenyekiti wa Kongamano la Kitaifa la Kujadili Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Shekh. Khamis Yussuf, akizungumza katika Kongamano hilo na kutowa maelezo juu ya Kongamano hilo linalojadili Rasimu hiyo, lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) jana.  
Mtoa Mada Shekh. Muhidin.akitowa mada katika Kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa SUZA, likizungumzia mustakabali wa Rasimu ya Katiba Mpya ya Tanzania. 
 Mwanasia wa Chama cha Upinzani Zanzibar, Rashid Joe, akichangia katika Kongamano hilo, lililoandaliwa na Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) akichangia mada iliowasilishwa na watoa Mada wawili, Ali Saleh na Shekh. Muhidin.
Mwananchi akichangia Mada katika Kongamano hilo la Kitaifa la kujadili Rasimu ya Pili ya Katiba.
 Akinamama wakiwa katika kongamano hilo.
Mmoja wa washiriki wa kongamano hilo, akichangia mada kuhusu Rasimu ya Pili ya Katiba.
Mmoja wa Mshiriki katika Kongamano la Kitaifa kujadili Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, akichangika katika kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa SUZA Vuga.
 Mshiriki wa Kongamano la Kitaifa lililoandaliwa na Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) akichangia katika kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha SUZA Vuga.na kuwashirikisha Wananchi na Maimamu. 

No comments:

Post a Comment