TANGAZO


Monday, April 21, 2014

Tamasha la Paska latikisa Uwanja wa Taifa

* Membe asema wananchi wataamua Serikali ngapi wanazitaka 

Mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernald Membe, aliyemwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika Tamasha la Pasaka, lililofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, akizungumza na mashabiki mbalimbali waliojitokeza katika tamasha hilo, aliwaomba kuwa watulivu wakati huu wa mchakato wa Katiba mpya, akisema uamuzi watautoa wao wananchi, ni Srikali ngapi wanazihitaji, ikiwa ni Moja, Tatu au Mbili, wao ndio wataamua na Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wao kazi yao ni kupitisha kile walichokiamua wananchi. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama na katikati ni Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Angela Kairuki.
Mwanamuziki wa muziki wa Injili kutoka Afrika Kusini, Keke Letse Phoofolo (katikati kushoto), akicheza na mashabiki wake wakati alipokuwa akitumbuiza katika tamasha hilo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana.
Mwimbaji wa muziki wa Injili kutoka Zambia, Ephraim Sekereti akiimba jukwaani wakati wa tamasha hilo jana.
Mwanamuziki wa muziki wa Injili kutoka Afrika Kusini, Keke Letse Phoofolo, akicheza na kwa mbwembwe wakati yeye na kundi lake walipotumbuiza kwenye tamasha  hilo.
Mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernald Membe, aliyemwakilisha Rais Jakaya Kikwete, akiongozwa kuelekea jukwaani na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama (kulia), uwanjani hapo jana.
Mwimbaji wa muziki wa Ijili kutoka Uingereza, Dayo Bello akiimba na mkewe Ruth Tobi, wakati wa tamasha la Pakasa, lililoandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana.
 Mwimbaji Jesca BM, akipagawisha mashabiki wa muziki huo, uwanjani hapo.
Mchungaji mtarajiwa, Masanja Mkandamizaji, akiwa na kundi lake, wakifanya vitu vyao uwanjani hapo.
Umati wa watu, ukiwa umejazana uwanjani hapoo kushuhudia tamasha hilo.
Mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernald Membe, aliyemwakilisha Rais Jakaya Kikwete kwenye tamasha hilo la Pasaka, akirejea kuketi huku akizungumza na Richard Kasesela na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama (katikati0, uwanjani hapo.
Msanii Upendo Kilahiro, akiimba jukwaani na kundi lake la Victoria Singers.
Mashabiki wa muziki huo, wakimshuhudia mwanamuziki Kekeletse Phoofolo (hayupo pichani), wakati alipokuwa akitumbuiza jukwaani hapo jana.
Msanii wa Muziki wa Injili, Upendo Nkone na kundi lake wakatumbuiza kwenye tamasha hilo.
Mwanamuziki wa muziki wa injili kutoka Afrika Kusini, Keke Letse Phoofolo, akiwa kazini.
Rose Muhando na kundi lake wakipagawisha kwenye tamasha hilo la Pasaka Uwaja wa Taifa, Dar es Salaam jana. (Picha zote kwa hisani ya Kamanda wa Matukio Blog)

No comments:

Post a Comment