TANGAZO


Monday, April 21, 2014

Chama cha Madaktari Wanafunzi Tanzania chatoa huduma za Afya Zanzibar

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Dokta Sira Ubwa Mamboya akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi katika uzinduzi wa kampeni za kutoa huduma za kisukari na shinikizo la damu zitakazofanyika Mikoa yote ya Zanzibar.
 Mratibu wa mtadi wa kutoa huduma za kisukari na shinikizo la damu Mr. Siraji M. Mtulia akitoa maelezo mafupi ya mradi huo utakaoanza kutekelezwa leo na Chama cha wanafunzi Madaktari Tanzania wakishikiana na Wizara ya Afya Zanzibar.
 Mkuu wa CHUO cha (IMTU) Prof. Flora Fabian akitoa maelezo kuhusu madaktari hao walivyojipanga kufanya kazi katika Mikoa yote ya Unguja na Pemba.
 Makamu wa Pili wa Rais Balozi. Seif Ali Iddi akiwahutubia Madaktari na wananchi waliofika katika uzinduzi wa kampeni za kutoa huduma za kisukari na shindikizo la damu huko ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Suza Mjini Zanzibar.
 Balozi Seif na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Sira wakikagua utoaji huduma mara baada ya kuzindua.
 Makamu wa Pili wa Rais Balozi. Seif Ali Iddi (wakatikati waliokaa) katika picha ya pamoja na wanafunzi madaktari kutoka vyuo mbalimbali Tanzania.
Balozi Seif akiagana na wanafunzi madaktari mara baada ya kuzindua huduma za upimaji afya katika sherehe zilizofanyika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Suza Mjini Zanzibar. (Picha zote na Makame Mshenga wa Maelezo, Zanzibar)

No comments:

Post a Comment