Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Daniel Lema akitoa mada juu ya changamoto zinazoikumba sheria ya kuzuia na kupambana na ukimwi nchini kwa washiriki wa semina iliyoandaliwa na TACAIDS hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa Tume ya kudhibiti ukimwi Nadhifa Omar (wa kwanza kushoto), akiwa miongoni mwa washiriki wa semina ya haki za binadam hivi karibuni jijini Dar es salaam.
Baadhi ya washiriki wa semina juu ya utekeleza sheria ya ukimwi ya 2008 na changamoto zake.
Washiriki wa semina ya wakifanya zoezi ili kuweka miili yao sawa kuendelea na semina.
Jaji Mstaafu kutoka nchini Kenya, Violet Mavisi akisisitiza juu ya haki zote anazotakiwa kuzipata mtu mwingine kwenye jamii, ni haki hizo hizo anazotakiwa kupata mtu anayeishi na virusi vya ukimwi katika semina iliyoandaliwa na TACAIDS kuwajengea uwezo mahakimu, maofisa wa polisi kutoka mikoa ya Dae es Salaam, Pwani na Morogoro pamoja wanasheria wa Serikali.
Baadhi ya washiriki wa
semina wakimsikiliza Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya kudhibiti ukimwi nchini
(TACAIDS) Dkt. Fatuma Mrisho wakati akifungua semina ya mahakimu, maofisa wa
polisi kutoka mikoa ya Dae es Salaam, Pwani na Morogoro pamoja wanasheria wa
serikali iliyoandaliwa na tasisi hiyo kwa watendaji wa Serikali hivi karibuni
katika ukumbi wa mikutano (Serengeti) jijini Dar es Salaam. (Picha zote na
Eleuteri Mangi- MAELEZO)
Na Eleuteri Mangi-
MAELEZO
MAAMBUKIZI ya virusi
vya ukimwi (VVU), yanazidi kupungua mwaka hadi mwaka Tanzania, kitu ambacho
kinaipa faraja ya tasisi ya Serikali inayosimamia masuala ya HIV/AIDS nchini.
Kauli hiyo, ilitolewa na
Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya kudhibiti ukimwi nchini Dkt. Fatuma Mrisho alipokuwa
akifungua semina iliyoandaliwa na tasisi hiyo kwa watendaji wa Serikali hivi
karibuni katika ukumbi wa mikutano (Serengeti), jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa semina
hiyo, walikuwa ni Mahakimu, Maofisa wa Polisi kutoka Mikoa ya Dar es Salaam,
Pwani na Morogoro pamoja wanasheria wa Serikali.
Semina hiyo, ililenga
kuwajengea uwezo watendaji wakuu wanaosimamia na kutekeleza sheria ya ukimwi ya
2008 katika kutimiza majukumu yao ya kila siku kwa kufuata sheri, kanuni na
taratibu kwa wanaohitaji msaada wa kisheria.
Dkt. Mrisho alisema
takwimu zinaonesha kuwa kwa ujumla maambukuzi ya ukimwi yamepungua kwa kiasi
kikubwa nchini ambapo zinaonesha kuwa Tanzania Bara na Visiwani kuanzia mwaka 2003 hadi 2004 yalikuwa ni
asilimia 7.
Mwaka 2007 hadi 2008 maambukizi
yalishuka mpaka kufikia asilimia 5.7 na mwaka 2011 hadi 2012 kiwango hicho
kilipungua zaidi na kufikia asilimia 5.1 ambacho ni kiwango cha kitaifa, wakati
Tanzani Bara pekee kiwango cha maambukizi ya VVU ni asilimia 5.3 zaidi ya kiwango cha kitaifa.
Taswira hii ya kupungua
kwa maambukizi ya VVU ni tumaini jema kwa nchi inayolenga kufikia uchumi wa
kati ifikapo mwaka 2025 kwani nguvu kazi inaonekana kuendelea kuimarika na
inawezekana kujenga uchumi imara kwa maendeleo endelevu.
"Kila mtu kwa
namna moja au nyingine anaguswa na ugonjwa wa ukimwi maana hakuna ukoo, kijiji,
wilaya na mkoa usio na mtu anayeishi na VVU na hivyo hadi nchi nzima inaguswa
na hali hiyo" alisema Dkt. Mrisho.
Kwa kuzingatia hali
hiyo, Dkt. Mrisho amewaasa washiriki hao wa semina na wananchi kwa ujumla kuwa
VVU kwa asilimia 80 huambukizwa kwa njia ya ngono, hivyo waache ngono zembe
zembe na kusimamia maadili ya kazi yao na ya kijamii ili maambukizi ya ukimwi
yaweze kupungua na kufikia kiwango cha asilimia sifuri hadi kufikia mwaka 2015
ambayo ni nia na lengo la TACAIDS na Serikali kwa ujumla.
Naye Mkuu wa Kitengo
cha Sheria TACAIDS Elizabeth Kaganda alisema kuwa watu wanaoishi na VVU ni
binadamu kama binadamu wengine ni lazima
waheshimiwe wapate mahitaji yao ya kila siku na tiba, mwathirika naye anapaswa
kumlinda mtu mwingine asipate ugonjwa wa ukimwi.
Kwa upande wake Jaji
Mstaafu kutoka nchini Kenya Violet Mavisi alisema kuwa ni wajibu wa mtu mmoja
mmoja kama raia, vyombo vya dola na
serikali kwa ujumla kujali haki za binadamu, kuzisimamia na kuzitekeleza
kulingana na sheria za nchi ikiwemo haki ya kuishi, kumiliki ardhi, kuoa, kolewa
na kuwa na familia na haki nyinginezo zinazotambulika kikatiba ndani ya nchi
husika.
Jaji huyo Mstaafu Kavisi
alisisitiza kuwa haki zote anazotakiwa kuzipata mtu mwingine kwenye jamii
usika, ni haki hizo hizo anatakiwa kupata mtu anayeishi na virusi vya ukimwi.
Mpaka sasa Tanzania kwa
hali ya maambukizi ya ukimwi mikoa inayoongoza kwa watu wanaoishi na kuishi na
VVU nchini ni 10 ikiongozwa na Njombe, Iringa, Mbeya, Shinyanga, Ruvuma, Dar es
Salaam, Rukwa, Pwani, Katavi na Tabora.
No comments:
Post a Comment