* Ni vipengele vinavyohusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na mipaka ya Tanzania
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Kapteni John Komba, akimueleza jambo mjumbe mwenzake, Said Arfi, nje ya ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma, baada ya kuaghirishwa kikao cha bunge hilo leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Zakia Meghji, akimuonesha jambo mjumbe mwenzake, Ole Sendeka, mjini Dodoma leo, wakati wakiwa tayari kuelekea kwenye Kamati zao kwa ajili ya kujadili Sura ya kwanza na ya sita za Rasimu ya Katiba kwenye kamati hizo, kabla ya kuwasilishwa rasmi siku ya Ijumaa kwa ajili ya kujadiliwa na kupitishwa kwa kupigiwa kura na wajumbe wa bunge hilo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka Zanzibar, wakielekea kwenye ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kuanza kikao cha kujadili Sura ya kwanza na ya sita za Rasimu ya Katiba, mjini Dodoma leo. Hata hivyo bunge hilo, liliaghirisha kujadili sura hizo, mpaka siku ya Ijumaa wiki hii.Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakiwa nje ya ukumbi wa Bunge, wakijadiliana masuala mbalimbali baada ya kuaghirishwa kujadiliwa kwa Sura ya kwanza na ya sita za Rasimu ya Katiba, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angela Kairuki na naibu mwenzake wa Viwanda, Biashara na Masoko, Janeth Mbene, nje ya ukumbi wa Bunge.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Margreth Sitta (kushoto), Dk. Mary Mwanjelwa (katikati) na Rita Mlaki wakifurahi, wakati wakijadili jambo nje ya ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Ismail Jussa Ladhu (kushoto), akiwaeleza jambo wajumbe wenzake, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba (kulia) na Dk. Aley Soud Nassor, nje ya ukumbi wa Bunge, mara baada ya kuaghirishwa kwa kikao cha bunge hilo leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Sheikh Mussa Kundecha (kushoto) na Mbwana Kibanda, wakijadili jambo, nje ya ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri wa Afya wa Zanzibar, Juma Duni Haji (kushoto) na Catherine Saruni (kulia), wakifurahi wakati mjumbe mwenzao, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar, Pandu Ameir Kificho, alipokuwa akifanya utani, nje ya ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Ismail Jussa Ladhu (kulia), akizungumza na waandishi wa habari, nje ya ukumbi wa Bunge, kuhusu masuala mbalimbali yaliyojitokeza, kwenye bunge hilo, aliyosema hawakubaliani nayo, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa bunge hilo, Samuel Sitta (kulia), akizungumza na waandishi wa habari, nje ya ukumbi wa Bunge, kuhusu masuala mbalimbali yanayolalamikiwa na wajumbe wa upinzani na baadhi ya wajumbe wengine, ambayo anadai wajumbe hao, hawakufuata ushauri wake na kusababisha kutokea hivyo, mjini Dodoma leo.
No comments:
Post a Comment