Muigizaji wa kike wa Hollywood Scarlett Johansson amekomesha
miaka yake minane kama balozi wa shirika la misaada ya kibinadamu la Oxfam.
Shirika hilo linamkosoa kwa kuunga mkono kampuni moja ya Israel inayoendesha
shughuli zake katika eneo linalokaliwa na walowezi la Ukingo wa Magharibi.Oxfam linasema kuwa uhusiano wa mwanasanaa huyo na Kampuni ya SodaStream iliyo na kiwanda katika eneo linalokaliwa na walowezi wa kiyahudi haiandamani na majukumu yake ya kuwa balozi wa kimataifa wa Oxfam
Hivi majuzi Scarlett Johansson alisaini mkataba na kampuni hiyo ya SodaStream na ataonekana katika matangazo ya kampuni hiyo wakati wa sherehe za American Superbowl mnamo siku ya Jumapili.
Oxfam inakataa biashara zozote kutoka kwa walowezi wa kiisrael, huku ikisema ni kinyume kulingana na sheria za kimataifa.
No comments:
Post a Comment