Mwili wa aliyekuwa mwandishi wa BBC aliyeaga dunia wiki jana
Ann Waithera umechomwa katika eneo la makaburi ya umma la Lang'ata mjini
Nairobi.
Ulikuwa wasia wa Ann aliyekuwa anapenda sana kutunza mazingira kuwa mwili
wake uchomwe na kisha majivu yake yatupwe kwenye mto na mengine kuwekwa katika
eneo ambako kutapandwa mti kama kumbukumbu kwake.Ann aliyekuwa na umri wa miaka 39 alifariki baada ya kuugua Saratani ya ubongo kwa miaka miwili tangu mwaka 2012.
Aliwahi kufanya kazi na mashirika mawili ya habari nchini Kenya, Nation na Citizen kama mtangazaji wa televisheni kabla ya kujiunga na shirika habari la kimataifa la BBC.
Katika BBC, alikuwa anafanya kazi kama ripota wa redio na televisheni hasa alipokwenda Ethiopia, kama ripota wa kwanza mwenye uwezo wa kuripoti katika lugha mbili, Kiswahili na Kiingereza.
Wakuu wa idhaa ya BBC Swahili David Okwemba, Ali Saleh na mkuu wa BBC Afrika Solomon Mugera wamemtaja Ann kama mchapa kazi na mfanyakazi aliyependa kujituma na kwamba BBC imepoteza mwandishi habari mahiri sana Afrika.
No comments:
Post a Comment