Bondia Husein Pendeza (kulia) wa Klabu ya Ashanti ya Ilala jijini Dar es Salaam, akimtupiana makonde na Ayubu Ibrahimu wa Green House wakati wa ufunguzi wa mashindano ya wazi ya Mkoa wa Dar es Salaam yanayoenderea katika ukumbi wa Panandipanandi, Ilala Bungoni jijini jana. Ibrahimu alishinda kwa point.
Mbunge wa Ilala Mussa Zungu akifuatilia mchezo huo wa ngumi.
Na Mwandishi Wetu SHILIKISHO la ngumi za Ridhaa, Mkoa wa Dar es Salaam umezindua rasmi mashindano yake ya kwanza tangu waingie Madarakani.
Mashindano yalifunguliwa jana na mgeni rasmi, Mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zungu na kukutanisha zaidi ya timu ishirini na mabondia 60 wa mkoa huo.
Akisoma risala kwa mgeni rasmi Mwenyekidi wa ngumi Mkoa wa Dar es Salaam, Akaroli Godfrey amesema mbali na mashindano hayo kuwa na changanmoto mbalimbali wameamua kuyafanya kwa kuwa yapo kwenye karenda yao ata hivyo akuna zawadi zozote kwa mabondia watakaopigana hivyo kama mbunge wa jimbo la ilala tunaomba utupatie angarau medali kwa mabondia aidha vifaa tulivyo navyo avikizi kimchezo.
Akijibu risara hiyo, Mbunge Zungu aliahidi kutoa zawadi pamoja na kuwa mlezi wa ngumi za ridhaa mkoa wa Dar es salaam na kuwasaidia kutafuta wadhamini mbalimbali watakaojitokeza kuinua mchezo wa masumbwi nchini ili ngumi zisonge mbele .
Katika mapambano ya ufunguzi huo, mabondia Antony Idoa alimtwanga kwa KO ya raundi ya pili bondia Mohamed Mzeru huku John Cristian akimsambaratisha Omar Said na Shabani Almasi akimdunda Saidi Kondo na bondia pekee kutoka timu ya Ashanti ya Ilala, Hussein Pendeza alipoteza kwa pointi kwa kuchapwa na Ayubu Ibrahimu.
|
No comments:
Post a Comment