TANGAZO


Tuesday, January 28, 2014

Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, azindua rasmi mradi wa Opportunity Tablets Shule ya Sekondari ya Nakayama, Rufiji mkoani Pwani

Bwana Joe Ricketts, Mwanzilishi na Rais wa Opportunity Education akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya WAMA Nakayama, Dkt Ramadhan Dau mara baada ya mgeni huyo kufika shuleni hapo tarehe 27.1.2014. (Picha zote na John Lukuwi-Idara ya Habari, Maelezo)
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Mwantumu Mahiza akisalimiana na Mwanzilishi na Rais wa Taasisi ya Opportunity Education yenye Makao Makuu yake huko Omaha katika Jimbo la Nebraska nchini  Marekani Bwana Joe Ricketts mara baada ya mgeni huyo kuwasili kwenye Shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama iliyoko wilayani Rufiji katika Mkoa wa Pwani tarehe 27.1.2014.
Mkurugenzi  Mkuu wa Mfuko wa Pensheni ya Mashirikia ya Umma, PPF, Ndugu William Erio akisalimiana na Bwana Joe Ricketts wakati wa mapokezi ya mgeni huyo aliyetembelea Shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama huko Nyamisati katika wilaya ya Rufiji. PPF ni moja ya Taasisi zinazofadhili shule hiyo. 
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete akimkaribisha rasmi Mgeni wake Bwana Joe Ricketts kwenye Shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama ambako kulifanyika uzinduzi rasmi wa Mradi wa Opportunity Tablets kwa shule hiyo na nyingine zilizomo kwenye mradi huo hapa nchini. 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea rasmi zawadi ya jezi ya klabu ya Chicago iliyoko nchini Marekani kutoka kwa Bwana Joe Ricketts, Mwanzilishi na Rais wa Taasisi ya Opportunity Education katika sherehe iliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama tarehe 27.1.2014.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa sherehe ya uzinduzi wa mradi wa Opportunity Tablets uliofanyika shuleni hapo tarehe 27.1.2014.
Mkuu wa Shule ya sekondari nya WAMA Nakayama Ndugu Tuma Mensa akitoa hutoba yake wakati  wa sherehe ya uzinduzi wa Opportunity  Tablets katika Shule hiyo tarehe 27.1.2014.
Bwana Jacob Julius, mmoja ya vijana waliofadhiliwa na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), katika masomo ya sekondari hadi  chuo Kikuu akitoa shukrani zake kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe ya uzinduzi wa Opportunity Tablets uliofanyika kwenye shule ya sekondari ya WAMA Nakayama iliyoko huko Nyamisati, mkoani Pwani tarehe 27.1.2014. 
Mwanzilishi na Rais wa Taasisi ya Opportunity Education ya mjini Omaha katika Jimbo la Nebraska nchini Marekani, Bwana Joe Ricketts akitoa hotuba yake wakati wa sherehe ya uzinduzi wa mradi wa  Opportunity Tablets kwa shule za hapa nchini uliofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama iliyoko wilayani Rufiji, mkoani Pwani tarehe 27.1.2014.   
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama wakicheza ngoma wakati wa sherehe za uzinduzi wa mradi wa Tablets.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama wakicheza ngoma wakati wa sherehe za uzinduzi wa mradi wa Tablets.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kwambwa akitoa hotuba yake kwa niaba ya serikali ya Tanzania wakati wa sherehe ya uzinduzi rasmi wa mradi wa Opportunity tablets iliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama tarehe 27.1.2014. 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea rasmi moja ya laptop 61kutoka kwa Mwanzilishi na Rais wa Taasissi ya Opportunuty Education ya nchini Marekani zilizotolewa kwa ajili ya Shule ya Sekondari ya  WAMA Nakayama katika sherehe iliyofanyika shuleni hapo tarehe 27.1.2014. Wengine katika picha, kushoto kwenda kulia ni Mkuu wa Shule ya WAMA Nakayama Ndugu Tuma Mensa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa na Mwenyekiti wa Bodi ya shule Dk. Ramadhan Dau.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikabidhi tablet moja ya tablet kwa mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama  tarehe 27.1.2014.
Mwanafunzi aliyekabidhiwa moja ya tablet huku akiwa na baadhi ya wanafunzi wenzake akiionesha kwa wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe hiyo huko Bwana Joe Ricketts akishuhudia. 
Mke wan a Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete akiwahutubia wanafunzi na wageni waalikwa wakati wa sherehe ya uzinduzi wa Opportunity Tablets uliofanyika katika Shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama tarehe 27.1.2014.
Mke wan a Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete akiwahutubia wanafunzi na wageni waalikwa wakati wa sherehe za uzinduzi huo.
Mke wan a Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete akihutubia wakati wa sherehe za uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete, akiwahutubia wanafunzi na wageni waalikwa wakati wa sherehe za uzinduzi huo.
Bwana Joe Ricketts akimpongeza Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwa hotuba nzuri aliyoitoa wakati wa sherehe ya uzinduzi wa tablets uliofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama huko Nyamisati, wilayani Rufiji tarehe 27.1.2014. 
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha pili wanaosoma katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya WAMA Nakayama wakifanya mazoezi mbalimbali kwa kutumia tablets zilizokabidhiwa kwenye 
shule hiyo mara baada ya uzinduzi rasmi uliofanywa na Mama Salma Kikwete tarehe 27.1.2014.    
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha pili wanaosoma katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya WAMA Nakayama wakifanya mazoezi kwa kutumia tablets zilizokabidhiwa kwenye shule hiyo mara baada ya uzinduzi rasmi uliofanywa na Mama Salma Kikwete tarehe 27.1.2014. 
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha pili wanaosoma katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya WAMA Nakayama wakifanya mazoezi kwa kutumia tablets hizo, zilizokabidhiwa kwenye shule hiyo mara baada ya uzinduzi rasmi uliofanywa na Mama Salma Kikwete tarehe 27.1.2014. 
Mmoja wa wanafunzi wa kidato cha pili wanaosoma katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya WAMA Nakayama wakielekezwa jinsi ya kuitumia tablets zilizokabidhiwa kwenye shule hiyo na mmoja wa wageni waliofika katika hafla hiyo.
Mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya WAMA Nakayama akimwonyesha Bwana Joe Ricketts na Mama Salma Kikwete namna ya kutumia tablet mara baada ya sherehe ya uzinduzi kwenye Shule hiyo tarehe 27.1.2013. (PIicha zote na John Lukuwi)

No comments:

Post a Comment