Mshindi wa Pikipiki katika Promosheni ya Timka na Bodaboda inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Salome Kalinga (wanne toka kushoto), mkazi wa Iringa,akipokea funguo wa pikipiki yake aliyojishindia katika promosheni hiyo toka kwa Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kusini Magharibi, Bw. Benedict Kitogwa. Ili kujiunga na Promosheni hiyo mteja anatakiwa kutuma neno PROMO kwenda 15544.
Meneja wa Vodacom Tanzania, Mkoa wa Iringa, Bw. John Watosha, akimfungia kamba za kofia ngumu Bw.Aloyce Mboya ambaye ni mmoja kati ya washindi(6)wa Promosheni ya Timka na Bodaboda wakati wa makabidhiano rasmi hapo jana,anaeshuhudia kulia ni Meneja Mauzo wa Mkoa huo Galus Baltazal.Ili kujiunga na Promosheni hiyo mteja anatakiwa kutuma neno PROMO kwenda 15544.
Mshindi wa Pikipiki katika Promosheni ya Timka na Bodaboda Mkazi wa Mkoa wa Iringa, Bw. Francis Mlelwa,akishuhudiwa na Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kusini Magharibi, Bw. Benedict Kitogwa (watatu toka kushoto), pamoja na washindi wenzake akiwa juu ya pikipiki yake tayari kwa kuondoka nayo mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Kaimu huyo,Ili kujiunga na Promosheni hiyo inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Mteja anatakiwa kutuma neno PROMO kwenda namba 15544.
Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kusini Magharibi, Bw. Benedict Kitogwa, akimkabidhi pikipiki, Bw. Francis Mlelwa ambaye ni mmoja kati ya washindi(6)wa Promosheni ya Timka na Bodaboda wakati wa makabidhiano rasmi mkoani humo hapo jana,Ili kujiunga na Promosheni hiyo mteja anatakiwa kutuma neno PROMO kwenda 15544.
Baadhi
ya washindi wa Promosheni ya Timka na Bodaboda wa Mkoa wa Iringa,wakiwa kwenye
picha ya pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Mkoani humo hapo jana mara
baada ya kukabidhiwa pikipiki zao za ushindi, ili kujiunga na promosheni hiyo
tuma neno Promo kwenda 15544.
Na Mwandishi wetu, Iringa
ZIKIWA zimebakia siku chache kwa Promosheni ya timka na bodaboda inayoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania kuisha, washindi kutoka sehemu mbalimbali za nchi wameendelea kukabidhiwa pikipiki zao safari hii ilikuwa ni zamu ya washindi sita kutoka kanda ya Kusini (Iringa) kukabidhiwa zawadi zao.
Akikabidhi pikipiki hizo sita Kaimu Mkuu wa Kanda Kusini Magharibi wa Vodacom Tanzania, Benedict Kitogwa aliwahimiza wateja wa mtandao huo kuendelea kucheza promosheni hiyo kwa kasi zaidi ukizingatia shindano hilo linakaribia kuisha mapema mwezi ujao.
“Promosheni hii ni yenye manufaa makubwa sana kwa wateja wetu ukizingatia inawasaidia kukabiliana na tatizo la usafiri linalowakabili watanzania na nchi kwa ujumla na pia kama njia mojawapo ya kuwaongezea kipato.” Alisema Kitogwa na kuongezea “Timka na bodaboda ni mkombozi wa watanzania na nimelishudia hilo, sasa watu wanamiliki biashara zao, hawana tatizo tena la usafiri na pia watu wanajishindia fedha ambazo wanaongezea mitaji yao na kujikwamua kiuchumi.”
Awali Meneja Mauzo Galus Baltazal na Meneja wa Vodacom Iringa John Watosha wamewapongeza washindi hao na kuwahimiza kuendelea kutumia mtandao wa Vodacom kila wakati.
Baadhi ya washindi wa Timka na Bodaboda waliopewa Pikipiki zao hapo jana ni Aloyce Mboya, Francis Mlelwa, Salome Kalinga na Hassan Ahmed Abdallah amboa kila mmoja alijishindia bodaboda moja.
Aloyce Mboya ambaye ni mshindi mmojawapo wa promosheni hiyo alibainisha kuwa sasa tatizo la usafiri kwake ni ndoto na pia anaweza kuitumia kama njia ya kujiingizia kipato.
“Ni furaha kubwa sana kwangu leo hii kukabidhiwa pikipiki hii kwani nimekuwa ni mteja wa Vodacom kwa muda mrefu na nimeshirika promosheni nyingi ikiwemo hii ya Timka na bodaboda. Nadhani kushinda kwangu leo naona ni kama zawadi kutoka kwa kampuni hii kwa kuwa mteja wa muda mrefu, nawataka wateja wa Vodacom kucheza promosheni hii na wasiojiunga na mtandao huu wafanye hivyo haraka kwani si tu wateja wake tunafaidi huduma bora za kimawasiliano bali pia tunaboreshewa maisha yetu.” Alihitimisha Mboya
Kujiunga na promosheni hii ni rahisi na mteja anachotakiwa kukifanya ni kuandika neno PROMO na kutuma kwenda nambari 15544.
No comments:
Post a Comment