Rais Jakaya Kikwete |
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anapenda kutoa mwaliko kwa makundi mbalimbali
kwa ajili ya kuwasilisha orodha ya watu wasiopungua wanne na waziozidi tisa kwa
ajili ya kuteuliwa kuwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kwa mujibu wa kifungu
kidogo cha (2A) cha kifungu cha 22 cha sheria ya Mabadiliko ya Katiba, sura ya
83 kinachomtaka Rais kuwaalika kila kundi lililoainishwa chini ya kifungu
kidogo cha (1) (c) kutoka pande zote za Muungano kuwasilisha kwake orodha ya
majina yasiyopungua 4 na yasiozidi 9 kwa ajili ya kuzingatiwa katika uteuzi.
Makundi
hayo ni kama ifuatavyo:
1.Taasisi
zisizokuwa za Kiserikali
2.Taasisi
za kidini
3.Vyama
vya siasa vyenye usajili wa kudumu
4.Taasisi za elimu ya juu
5.Makundi
yenye ulemavu
6.Vyama
vya wafanyakazi
7.Vyama
vinavyowakilisha wafugaji
8.Vyama
vya wakulima
9.Vyama
vinavyowakilisha wavuvi
10.Makundi mengine yenye malengo
yanayofanana
Katika
kuwasilisha majina hayo, makundi yaliyoalikwa yatalazimika kuonesha umri,
jinsia, uzoefu, sifa na sehemu ya makazi ya mtu aliyependekezwa ikiwa ni pamoja
na kuzingatia usawa wa kijinsia.
Mheshimiwa
Rais ameelekeza kuwa orodha ya majina yanayopendekezwa yawasilishwe kwa maandishi
ama kwa kupeleka kwa mkono au kutumia huduma ya posta kwa anuani zifuatazo:
1.Katibu
Mkuu Kiongozi,
Ofisi ya Rais, Ikulu,
S.L.P. 9120,
DAR
ES SALAAM
2.Katibu
Mkuu Kiongozi,
Ofisi ya Rais,
S.L.P. 4224,
ZANZIBAR
Mwisho
wa kupokea orodha ya majina hayo nitarehe
02 Januari, 2014.
No comments:
Post a Comment