Rais wa Marekani, Barack Obama ameonya kuwa Sudani kusini iko
katika hatari ya kuingia katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, baada ya
kutokea mapigano mjini Juba.
Amesema kuwa Wanajeshi 45 wamepelekwa nchini Sudani kusini siku ya jumatano
kwa ajili ya kuwalinda Raia wa Marekani na mali zao.Takriban watu 500 wanahofiwa kupoteza maisha tangu mwishoni mwa juma lililopita, wakati Rais wan chi hiyo Salva Kiir alipomtuhumu aliyekuwa makamu wake Riek Machar kwa kutekeleza jaribio la kupindua Serikali.
Walinda Amani wenye asili ya India waliuawa siku ya Alhamisi kambi ya Umoja wa Mataifa inayohifadhi wakimbizi iliposhambuliwa katika eneo la mpaka kati ya Sudani kusini na Ethiopia, jimboni Jonglei.
Akitoa taarifa kuhusu vifo hivyo katika mkutano wa UN jijini New York, Balozi wa India ndani ya UN Ashok Mukeriji amesema kuwa mashambulizi ya siku ya Alhamisi yaliyotekelezwa na vijana wa jamii ya Nuer katika kambi yao yaliwalenga wao .
Sudani ilipitia kipindi cha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka 22,mapigano yaliyogharimu maisha ya Zaidi ya watu milioni moja kabla ya Sudani kusini kupata uhuru wake mwaka 2011.
Mgogoro wa sasa unahusisha jamii ya Nuer anakotoka Machar na Dinka anakotoka Kiir.
Machar amekana shutma kuwa alikuwa na mipango ya kuipindua Serikali ya nchi hiyo.
Ingawa wito umekuwa ukitolewa kutaka utulivu miongoni mwa makundi hayo hasimu, bado mapigano yameendelea katika mji wa Bor jimbo la Jonglei kaskazini mwa Juba.
Msemaji wa Umoja wa Afrika Ateny Wek Ateny amesema kuwa mji wa Bor unadhibitiwa na vikosi vitiifu kwa Machar hata hivyo Vikosi vya Serikali vinafanya jitihada ya kuurejesha mji huo kwenye himaya yao.
No comments:
Post a Comment