Kesi inayomkabili Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta huenda
ikachelewa kuanza baada ya mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya kimataifa ya
uhalifu wa jinai (ICC) Kukiri kuwa hana ushahidi wa kutosha wa kuendeleza kesi
hiyo.
Rais wa Kenya amekanusha mashtaka ya dhulma dhidi ya ubinadamu zinazohusiana
na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007. Zaidi ya watu elfu moja
waliuawawa katika mapiganao hayo na maelfu yaw engine kupoteza makazi yao.Kujiondoa kwa mashahidi hao imemfanya kiongozi wa mashtaka kusema kuwa kesi dhidi ya Bwana Kenyatta haifikii kiwango cha ushahidi kinachohitajika jambo lililomchochea kuomba kesi hyo isimamishwe kwa muda ili aweze kusawazisha na kukusanya ushahidi zaidi.
Kesi ya Bwana Kenyatta ilipaswa kuanza huko The Hague tarehe 5 Februari mwaka ujao . Bwana Kenyatta alishtakiwa pamoja na naibu wake William Ruto na mtangazaji Joshua Arap Sang kwa makosa ya mauji, kusababisha watu kuhamishwa kwa nguvu katika makazi yao, kusababisha mateso kwa umma na ubakaji kufuatia ghasia zilizotokana na matokeo ya urais katika uchaguzi huo.
Kesi ya Kenyatta na naibu wake imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu na jamii ya kimataifa haswa baada ya Umoja wa Afrika kutishia kuyaondoa mataifa ya Afrika katika uanachama wa mahakama hiyo iliyobuniwa chini ya mkataba wa Roma. Umoja wa Afrika umekuwa ukidai mahakama hiyo imekuwa ikiwalenga viongozi wa bara Afrika.
No comments:
Post a Comment